Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Wednesday, August 5, 2009

kijana orton sr




RANDY Orton ni mmoja kati ya wababe wanaotamba katika ulingo wa mieleka na ni kivutio kizuri kwa mashabiki wengi wa mchezo huo.

Kama ilivyo kwa wachezaji wengine mbabe huyo pia ametokea katika familia ya mieleka ambako babu yake, Bob Orton Sr alikuwa mchezaji na baba yake Bob Orton Jr. amekuwa akionekana mara kwa mara katika mechi za kijana wake ikiwa ni pamoja na kuingilia pindi kijana wake huyu anapoonekana kuzidiwa.

Kihistoria mbabe huyo jina lake halisi ni Randal ‘Randy’ Keith Orton, akiwa amezaliwa April 1, 1980, akiwa na uzito wa kilogramu 111.

Kabla ya kujiunga moja kwa moja WWE alianzia katika vyama vya Mid-Missouri Wrestling Association-Southern Illinois Conference Wrestling kwa muda wa miezi kadhaa.

Baada ya kufanya vema alijiunga na chama cha Ohio Valley Wrestling (OVW). Ambako alifanikiwa kutwaa ubingwa wa OVW Hardcore.

Kutokana na uwezo wake mzuri alijikuta WWE, ikimuingiza Orton moja kwa moja katika chama hicho cha WWE.

Katika mwezi huo wa kwanza wa kujiunga kwake aliwashangaza mashabiki kwa kutwaa ubingwa wa mabara wa WWE.

Mwaka 2004, Orton alifanikiwa kuandika historia ya kuwa bingwa mdogo kabisa kutwaa taji la ubingwa wa uzito wa juu, akiwa ametwaa ubingwa huo akiwa na umri wa miaka 24.

Mwaka 2006, akiwa katika timu moja na Edge iliyokuwa ikijulikana kama Rated-RKO. Walifanikiwa kutwaa ubingwa wa timu wa dunia wa Tag.

Baada ya kuachana kwa timu hiyo katikati ya mwaka 2007, Orton alifanikiwa kutwaa ubingwa wa WWE mara mbili katika usiku mmoja.

Kwa sasa ndiye bingwa wa mashindano makubwa ya Royal Rumble.

Orton akiwa amezaliwa Aprili 1, 1980 huko Knoxville, Tennessee na mwanamama Elaine na mumewe mcheza mieleka ‘Cowboy’ Bob Orton.

Katika makuzi yake alionekana kuwa mpenzi wa mchezo wa mieleka lakini mara zote mzee wake alikuwa akimuonya kuhusu mchezo huo akimwambia kucheza mchezo huo ni sawa na kuyaweka maisha yake rehani.

Baba yake alimkazania kusoma ambako alijitahidi kumsomesha lakini akiwa katika kidato cha sita alijikuta akipuuza mawazo ya baba yake na hatimaye kujiunga na mieleka ya ridhaa.
Baada ya kuhitimu mwaka 1998, alijiunga na kikosi cha jeshi cha Maji, ambako hakuweza kudumu sana katika kazi hiyo kutokana na kuonyesha utovu wa nidhamu kwa makanda waike.

Baada ya kurejea nyumbani mwaka 2000 baba yake alianza kumfua kwa ajili ya kucheza mieleka ili aweze kujipatia kipato kutokana na kijana wake kuonyesha kuhuusudu mchezo huo.

Mwaka 2001, Orton alisaini dili la kucheza (WWE) .

World Wrestling Entertainment

Mechi yake ya kwanza akiwa WWE ilimkutanisha na Stevie Richards aliyofanikiwa kumpiga katika raundi ya kwanza.

Baada ya kumalizika kwa pambano hilo, alishinda lakini likimuacha na majeruhi ya mguu ambayo alikaa kwa muda na baada ya kupona aliibuka na kujiunga na timu ya Evolution stable, iliyokuwa inawajumuisha wababe kama Ric Flair, Triple H na Dave Batista.

Orton akitumia staili ya RKO, alifanikiwa kushinda mechi kibao hata ile iliyomkutanisha na mbabe Rob Van Dam alifanikiwa kumvua ubingwa wa mabara wa WWE katika mechi iliyochezwa Desemba 14, 2003.

Baada ya kupata mkanda huo aliweka historia ya kukaa nao kwa muda mrefu uliofikia miezi saba.

Mwaka 2004, alimchapa mchezaji wa zamani wa mieleka Mick Foley na kutetea ubingwa wake wa mabara.

Baada ya miezi saba kupita akiwa na mkanda huo alinyang’anywa na baada ya kunyang’anywa aliandika historia nyingine ya kutwaa ubingwa wa uzito wa juu wa dunia wa WWE akiwa kijana mdogo kuliko wote waliowahi kuutwaa akiwa na miaka 24.

Januari 2005, akicheza mashindano ya Royal Rumble, Triple H alimshinda Orton na kutwaa ubingwa wa WWE.

Akicheza dhidi ya Batista, alifanikiwa kutwaa ubingwa wa uzito wa juu wa dunia.

Mwaka 2005 akicheza dhidi ya Undertaker, baba yake Bob Orton alijikuta akiingilia baada ya kuona Undertaker akimzidia mwanaye alimsaidia na kumshinda mbabe huyo na kumuingiza katika jeneza.

Januari 2006, akicheza mashindano ya Royal Rumble akicheza dhidi ya Rey Mysterio, lakini alijikuta akishindwa kufurukuta kwa Mysterio ambaye alimshinda na kutwaa taji la WWE.

Katika mechi ya marudiano Orton alifanikiwa kutwaa ubingwa wa juu wa WWE kwa kumchapa Mysterio.

Julai 23 Orton alitwaa ubingwa wa WWE baada ya kumpiga mbabe John Cena kwa taabu ikiwa ni wiki tatu baada ya Cena naye kumapa kichapo cha nguvu.

Walirejea baada ya wiki mbili na Orton alijikuta akichezea kichapo toka kwa Cena. Katika mechi iliyofuata Orton alifanikiwa kushinda baada ya kusaidiwa na baba yake, Bob Orton.

Orton baada ya kushinda ubingwa wa 2009 wa Royal Rumble dhidi ya Jeff Hardy.

Novemba 2005, Orton alitangaza nia yake ya kumuoa, Samantha Speno aliyemuoa Septemba 21, 2007 na Desemba 2007, walipata mtoto wao wa kwanza wa kike anayeitwa, Alanna Marie Orton.

Jamaa huyu katika mkono wake wa kushoto amejichora ‘tattoo’ iliyo na maandishi yanayosomeka ‘USMC’ ikimaanisha, Jeshi la Maji la Marekani akikumbuka mateso aliyoyapata.

Nyanja ya muziki ameshatoa vibao kama ‘Voices’ akiwa na Rev Theory, ‘This Fire Burns’ akiwa na Killswitch Engage .

Vingine ni ‘Burn in My Light’, ‘Line in the Sand’, ‘Evolve’ akiwa ameshirtikiana na Jim Johnston na ‘Blasting’.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text