Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Thursday, December 13, 2007

MUZIKI WA HIP HOP UNAUZA HASA MSANII MAKINI

MUZIKI wa Hip Hop ni nini? ni muziki wa kurapu au kufoka au kukaripia hasa kwa nia ya kuzuia uonevu, unyanyasaji au ubaguzi wa aina yoyote kwa binadamu mwenzako.

Mwanzoni mwa mwaka 1960 muziki huu ulikuwa ukitumika kama utamaduni wa mtu mweusi kwenye maeneo ya Kingstone, Jamaica.

Na katika mwaka 1970 ulionea maeneo ya South Bronx na jijini New York huko Marekani kwa wamarekani weusi waliokuwa wakipinga vitendo vya kibaguzi kutoka kwa wazungu ikiwa ni pamoja na kupinga siasa inayoonyesha kuwashusha wao kutokana na rangi yao.

Kutokana kukua kwa muziki huo ndipo ikawa mwanzo wa kuzaliwa kwa mitindo kama Dancehall, R&B, disco, funk na mingineyo ambayo ipo sasa kiini chake ni Hip hop.

Mambo yaliyokuwa yakizingatiwa katika kuuwakilisha muziki huu wa Hip hop yalikuwa ni lazima wafanyaji wa muziki huu wawe na vitu kama Kikalio cha Santuri, mashairi, ngoma, Santuri ya kusugua, upangiliaji wa Vina na mizani na Dj.

Baada ya kuenea zaidi nchini Marekani miaka ya 1980 nchi hiyo ilifanikisha kuutangaza vilivyo na kufanya hata kusambaa dunia nzima miaka ya 1990.

Baada ya kuonekana kuwa juu zaidi muziki huu ulianza kugawanywa katika makundi mbali mbali hapo wakatokea wasanii waliokuwa wakiimba rapu iliyokuwa katika staili za Abstract, Alternative, Chopped , screwed, Christian, Conscious, Crunk, Gangsta, G-funk, Hardcore, Horrorcore, Hyphy, Instrumental, Jazz rap, Latin rap, Mobb, Nerdcore, Old school, Pop rap na Snap.

Baadhi ya mambo yanayofanywa na wana hip hop wa kiukweli ni kurapu bila ala ‘uimbaji wa akapela’ (Freestyle) kuchora, ‘kuruka majoka’ (kucheza ‘Breakdancing’), kushirikiana, madj wanaosugua santuri, uvaaji wa kawaida, kusoma historia ya mtu mweusi.

Muziki huu wa Hip hop umegawanyika katika makundi matatu la kwanza ni Roots, Old School na Golden Age ( ambayo ni ya miaka hii) ambayo wengi wa wanaharakati wanadai kuwa imekomea miaka ya 1990.

Baadhi yao wamekuwa na dhana kwamba muziki huu hauenziwi tena kama mwanzo kutokana na wengi wa wasanii kuvunja miiko yake na wapo wanaodai kuwa muziki huu bado upo hai kutokana na ukweli kwamba muziki huu si muziki kama unavyoonekana kijujuu ila ni utamaduni hivyo kuisha kwake ni mpaka waafrika wapotee katika uso wa dunia.

Kundi la kwanza la Old School Hip Hop hili ni la miaka ya 1979 hadi 1985 wasanii wake walikuwa ni wale waliokuwa wakifoka kwa kufuata midundo na baadae walipewa jina la ‘MCs’ au ‘emcees’ kazi zao walikuwa wakizifanyia jukwaani peke yake.

Katika kundi hilo kulikuwa waanzilishi waliopata kuvuma kama akina DJ Kool Herc, Coke La Rock na Clark Kent walikuwa wakirapu kwa mtindo wa Country.

Baadae kukawa na kundi kubwa la wana Hip hop waliokuwa wakiimba mitindo ya ‘kigang’ (kigumu) lilikuwa na wanachama kama Afrika Bambaataa's Universal Zulu Nation.

Kizazi kingine kilikuwa cha miaka ya 1986 hadi 1997 kilichojulikana kama ‘Golden age hip hop’ ambayo iliwatambulisha wasanii kama Run-D.M.C.'s walifikia hatua hadi ya kutoa albamu iliyojulikana kama Hell mwaka 1986.

Hapa miaka hii ilifunguliwa studio binafsi iliyojulikana kama Def Jam Recordings iliyosaini mikataba na baadhi ya marapa.

Hapa baadhi ya marapa walivumbuliwa kama Big Daddy Kane na Kool G Rap aliyekuwa kwenye studio ya Cold Chillin' Records na Eric B & Rakim.

Mwaka 1984 msanii kama Ice-T akatoka na wimbo ‘Killers’, mwaka 1988 kundi la Public Enemy likaachia wimbo ‘It Takes a Nation of Millions to Hold Us Back’.

Katika mwaka huo marapa kama DJ Jazzy Jeff na The Fresh Prince (Will Smith) walishinda tuzo za kwanza za Grammy kwa kuwa wasanii bora wa rapu.

Mwaka 1998 wasanii kama Ice T, N.W.A wakiwa kama waasisi wa rapu aina ya Gangsta walifanikiwa kuitambulisha vilivyo aina hiyo ya Hip hop kwa mashabiki wao.

Mtindo huo ulikuja kuwa maarufu sana miaka ya 1990 kwa kudakwa na marapa kama Marehemu Notorious B.I.G., Puff Daddy, Eazy E, Dr. Dre, Bone Thugs N Harmony, Snoop Doggy Dogg na Marehemu Tupac Shakur.

Miaka ya 1990 muziki huu ulibadilika na sasa wanauita New School muziki wa kizazi kipya kuanzia mwaka 1998
Ambao umeshika chati miongoni mwa wasanii wengi wachanga kutoka nchini Marekani.

Tofauti na wanamuziki wa mwanzo hawa wa sasa wakaanza kutangaza zaidi ‘unyukaji wa pamba’ kuvaa vipuri, cheni, pete za dhahabu kwa marekani staili hii inajulikana kama ‘Jiggy/bling rap music’.

Kitu kilichonifanya nizungumzie mada hii ya Muziki wa Hip hop imetokana na mapenzi niliyonayo na muziki huu mara baada ya kusikia wimbo wa kiongozi wa kundi la Tip Top Connection Organization (TTCO), msanii Madee Seneda unasema kuwa ‘Hip hop haiuzi’.

Kweli maneno aliyoyatumia ndani ya wimbo huo hayakuwa ya busara ya kudai kuwa haiuzi ni bora ya muuza pipi kuliko muimbaji wa Hip hop.

Hii inatokana na yeye kufanya muziki huo kwa muda mrefu huku ajui historia ya muziki huo vizuri ndicho kisa alipotaka kubadili staili akasema kwamba ameacha Hip hop na kumbe hajui kuwa hata kuimba hivyo nayo ni Hip hip ila tu inabadilika pale ambapo atakapo jaribu kuyimba uongo hiyo ndiyo itakuwa imekwenda kinyume na Hip hop.

Madee anastahili kutambvua kuwa muziki huu unabadilika kulingana na wakati kama tulivyoona juu kuwa Hip hop ndiyo mzizi wa mitindo ya R&B, DanceHall, Rapu, Disco dance.

Kitu kilichonisikitisha na kumuona kuwa Madee hajui alichokuwa akikiimba kwenye wimbo wake huo kuwa ameachana na Muziki wa Hip hop kuwa hauuzi sasa, sasa cha kujiuliza ni kwamba iwapo miziki yote kiini chake ni Hip hop sasa yeye atakuwa anaimba kitu gani?.

Napenda kumueleza Madee kwamba hapa nyumbani wapo wasanii wengi wanaoimba Rapu na wamefanikiwa na kupata sifa kubwa kwa mfano baadhi ya wanaofanikiwa kwa kupitia muziki huu ni kama, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, John Simion ‘Joh Makini’, Nako 2 Nako Joseph Mbilinyi ‘Mr II maarufu kama Sugu’.

Hivyo natoa ushauri kwa Madee atambue kuwa Hip hop inauza hasa kwa mtu makini na iwapo hayupo makini bado ataendelea kutapatapa iwapo akiendelea kuzunguka bila kuchukua uamuzi sahihi.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text