NENO Bongo fleva husimama kumaanisha aina ya muziki wa kizazi kipya unaofanya na wasanii wa kizazi kipya,hususani vijana huku wengine wakitumia staili za kughani(kurap) na wengine wakiimba kwa lugha za kiswahili.
Katika hili limekuwa likizua utata kwa baadhi ya wasanii wakikataa kujumuishwa kwenye majina ya wasanii wa Bongo fleva kwa kile wanachodai kuwa waowanafanya Hiphop na sio Bongo fleva na kuacha utata mkubwa huku baadhi ya mashabiki na wadau wakiwa hawajui kutofautisha kati ya Bongo fleva na Hiphop.
Msanii tuanae muangalia leo ni mmoja kati ya anayefanya aina ya Hiphop na sio Bongo fleva,hili ni kutokana na aina za midundo na dhamira zinazopatikana kwenye nyimbo zake pamoja na aina anayoitumia katika mwenendo wa maisha yake.
Huyu sio mwingine bali John Simon Mseke anayejulikana zaidi kama 'Jo makini', msanii anayetokea Mkoani Arusha ambaye yeye mwenyewe kwenye nyimbo zake hupenda kujitambulisha kwa jina la mwamba
wa kaskazini.
Kwa hivi sasa hapa nchini unapowataja wasanii wanaofanya Hiphop hapa nchini,Jo makini ni mmoja kati ya wanahiphop ambao wapo juu kileleni akifanya vizuri na nyimbo yake inayotamba kwa hivi sasa inayokwenda kwa jina la 'Mfalme'.
Mfalme ni baadhi ya singo ambayo ipo hewani ikiiwakilisha albamu mpya ya msanii huyu ambayo tayari imeshakamilika huku ikisubiira taratibu mablimbali za kuweza kuitamburisha rasmi na kuipeleka sokoni.
Hivi karibuni Changamoto liliweza kukutana na msanii Jo makini na kuielezea albamu yake mpya kwa ufupi pamoja na kuelezea historia yake ya kimuziki.
Akiielezea albamu yake mpya Jo makini anasema kuwa albamu hiyo tayari amesharekodi nyimbo kama ishirini katika studio mbalimbali,lakini atazichuja na kupata nyimbo kumui na mbili ambazo ndio zitaingia kwenye albamu yake hiyo mpya na ya pili kwa msanii huyu.
Akiwataja wasanii aliofanya nao kazi Jo makini kwenye albamu yake mpya ni kama 'Ambrose' aliyeshirkia kwenye nyimbo
ya 'Sijutii',Niki kwenye 'bado sijamaliza',Enika kwenye 'ulimwengu wa wapendanao'Fatuma kwenye nyimbo ya'Mfalme',wasanii wengine alioshirikia nao ni kama Adili na Magazijuto.
Jo makini watu wengi walianza kumjua pale alipoibuka na nyimbo yake ya 'Hao',aliyokuwa ameitoa mwaka 2005,chini ya utayairishaji wake 'producer Ludigo',na kuweza kumtambulisha vizuri kwenye medali za Hiphop za wasanii wa hapa nyumbani.
Lakini akielezea historia yake ya kimuziki Jo makini anasema,muziki aliuanza miaka ya tisini kati ya 1995 na 1996,wakati huo akiwa na msanii mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Yusuph.
Akielezea wasanii anao wapenda Jo makini anasema waliomvutia na wanao endelea kuwapenda duniani ni msanii Nas escoba,Jay Z a.k.a. Jigga, na marehemu 2 Pac,ambaye ndio bingwa gwiji wa Hiphop hapa duniani.
Lakini mkazo zaidi kwenye muziki aliweka kwenye mwanzoni kabisa mwa miaka ya 2000 alipokuwa amejiunga na wasanii wenzake na kuunda kundi la 'River soldier
camp',akiwa na wasanii wenzake kama Ras omega,Bonda ba wengineo wengi.
Mnano mwaka 2001,mwamba wa kasikazini alifanikiwa kuingia studio na kutoa nyombo yake iliyojulikana kwa jina la 'Umasiki',ndani ya studio za Mj records,nyimbo ambayo ilitayarisha na 'producer Ludigo.
Mwaka 2002,Jo makini aliingia tena studio akiwa na wenzake wa River soldier camp na kutoa nyimbo yao iliyokwenda kwa jina la 'Mambo mchanganyiko',ingawa haikuweza kuwatambulisha vizuri sana kwenye Hiphop.
Baada ya hapa aliendelea kutoa nyimbo zake peke yake ambapo kwenye mwaka 2004,aliibuka na nyimbo yake ya 'Hawapendi',na 'Basi tufanye tumoro',kabla ya kutoa nyimbo ya 'hao 'ambayo ndio ilimtambulisha vizuri 2005.
Mwaka 2006 alitoka na nyimbo yake ya 'Chochote popote',ambayo ndio ilimpa umaarufu zaidi nyimbo ambayo kabla ya kutoka na nyimbo yake nyingine ya 'Zamu yangu',ambayo nayo ilimpa uhakika wa kuwekwa kwenye ramani ya wasanii wa Hiphop hapa nchini na kufanikwa kuiwakilisha vizuri ramani ya
Arusha.
'Zamu yangu' ndio nyimbo ambayo ilikuwa imebeba jina la albamu na kumuwezesha msanii huyu kuipeleka kwa wahindi ambapo kila kanda yake moja iliuzwa kwa shilingi mia mbili.
Kama ilivyo kwa wasanii wengi wa Bongo fleva na Hiphop hapa nchini,Mwamba wa kasikazini ni moja kati ya wasanii wanaolalamika kutoridhika na maripo wanayoyapata kutoka kwa wahindi kariakoo kwa kulipwa malipo madogo mno kwenye kanda zao wanazoziuza kwa wahindi hao hapo kariakoo.
Pamoja na kupanda kwagharama za kimaisha na kushuka kwa dhamani ya shilingi ya kitanzania,bado wasanii wanalipwa fedha ndogo huku kanda za kaseti za nyimbo zao zikiuzwa kati ya shilingi 1200 hadi 1500 kwa kanda moja lakini msanii analipwa shilingi 200 hadi 250.
Kilio chake Jo makini ni kwa Serikali kuweza kuwasaidia kwa kuweka viwango maalumu vyenye unafuu wa kazi zao wanazoziuza kwa wahindi hao,ili kuweza kuokoa maendeleo ya wasanii na taifa kwa ujumla.
Lakini pamoja na hayo bado Jo makini
anawalaumu wasanii wenzake kwa kutokuwa na ushirikiano wa kutosha wa kuweza kuritokomeza suala hili na kusababisha linakuwa tatizo la kudumu hapa nchini na kuacha kilio cha kila siku kwa wasanii.
Akielezea ndoto zake Jo makini ni mmoja kayi ya wasanii wenye ndoto za kuja kumiliki studio yake mwenyewe kama ilicyo kwa wasanii wengi nchi wanavyomiliki stdio zao wenyewe ama dunia kwa ujumla.
Jo makini anawaondoa shaka wale wote wenye imani ya kuwa wasanii wa Hiphop kutoka Mkoani Arusha hawana uhasama wa mtafaruku wowote kama ambavyo imani za watu zilivyo kwa kuona ushirikiano wao mdogo.
Jo makini anasema yeye na wasanii wenzake wa Arusha wanaishi freshi kwa amani akiwa na ushirikiano wa dhati na wasanii kama Nako 2 nako,Mapacha na wengine wote.
Ingawa

0 comments:
Post a Comment