SALAAM aleyikum ndugu zangu Waislamu na wasio Waislamu kwa kuendelea kutimiza nguzo ya nne ya Uislamu ya Funga, leo ikiwa ni ramadhani ya 14.
Tunaendelea kukumbushana kama alivyotufundisha Mtume wetu (SAW) kuwa ‘kwa Waislam ukumbusho ni dawa’.
Leo katika mada ya leo tunaelezana faida za mwenye kufunga kiroho na kiafya, kwa sababu wapo baadhi ya watu hufikiria kufunga ni mateso au manyanyaso kwa mfungaji.
Faida za kufunga zipo nyingi, miongoni mwao ni kutekeleza mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu alizotuteremshia na faida ya utekelezaji huu ni kuingia peponi siku ya mwisho.
Faida ya pili ya mfungaji wa Swaumu ni kujizoesha kuwa na subira, yaani katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mtu anajifunza jinsi ya kuwa mvumilivu na kustahamili njaa, kiu na matamanio ya kimwili.
Mtume (SAW) anausifia mwezi huu kwa kusema kuwa: “Huo mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kusubiri na hakika subira malipo yake ni pepo”.
Faida ya tatu kwa mfungaji ni kuwa muadilifu na kujifundisha usawa baina ya tajiri na maskini.
Kwa hali ya kawaida tajiri ni nadra kushinda njaa, hivyo basi pindi anapokuwa katika swaumu anajua machungu ya njaa hata anapofikiwa na masikini akiombwa msaada na mtu mwenye njaa aweze kumsaidia kirahisi akiwa anafahamu namna njaa inavyouma.
Iwapo tajiri ambaye hajawahi kushinda njaa inakuwa ni vigumu kwake kusikia uchungu na kuwa mwepesi kumsaidia mwenye njaa kwa sababu anachukulia kama jambo la kawaida.
Kuhusu hilo la kufunga, lmam Ja'far Assadiq, amelizungumzia na kusema: “Hakika si jingine, Mwenyezi Mungu amefaradhisha kufunga ili wapate kulingana tajiri na maskini (katika shida ya njaa na kiu), basi akapenda viumbe vyake wawe sawa na amuonjeshe tajiri maumivu ya kushikwa na njaa ili apate kumhurumia mnyonge na apate kumsikitikia mwenye njaa”.
Faida ya nne na ambayo ni muhimu zaidi wanayoitegemea ni kusamehewa dhambi yote ya mwaka ikiwa mwenye kufunga amefuata masharti yote na kufunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama alivyosema Mtume (SAW) katika moja ya hotuba alizozitoa katika mwezi huu.
Anasema kuwa: “Enyi watu! Hakika umewaelekeeni nyinyi mwezi wa Mwenyezi Mungu (mwezi wa Ramadhani) kwa baraka, rehema na msamaha, mwezi ambao ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko miezi yote, siku zake ni bora kuliko siku zote, masiku yake ni bora kuliko masiku mengine yote na saa yake ni bora na muhimu kuliko saa zote”.
Hivyo kutokana na maneno hayo ya kipenzi chetu, Mtume (SAW), anaonyesha kufunga kwa Muislam katika mwezi huu ni bora na heri kwake.
Faida ya tano ya Swaumu inahusu upande wa afya zetu, kwa kawaida chochote kifanyacho kazi sharti kipumzike kwa muda, hii inajumuisha hata kwa upande wa mitambo.
Kwa mfano, mitambo ambayo imeundwa kwa vyuma imara tena vyenye nguvu hufika wakati ambao huwalazimu kusimama kwa marekebisho ili ifanyiwe ukarabati wa kuiendesha kwa ubora.
Swali hapa linakuja, kwa nini sisi ambao tumeumbwa dhaifu tusivipumzishe viungo vyetu, na hasa tumbo ambalo huendelea na kazi mfululizo kwa miezi 11? Hapo utauona ulazima wa kuyapumzisha matumbo yetu ili kuhifadhi afya zetu.
Kuhusu hilo la kusaidia kiafya hata madaktari wakubwa duniani wamewahi kulizungumzia hilo la kufunga.
Baadhi ya madaktari wakuu ulimwenguni, wamekaririwa wakithibitisha kuwa kunafaida kwa mfungaji na hata Mtume wetu (S.A.W.) anathibitisha hilo pale anaposema: “Fungeni ili mpate afya nzuri”.
Naye Imam Ja'far (AS) anasema, “Kila kitu kina utakaso, kitakaso cha mwili ni kufunga (Swaumu).
Kwa mujibu wa daktari mmoja mkubwa kutoka Marekani Dk. Car amewahi kusema kuwa “Ni wajibu juu ya kila mgonjwa ajizuie kula japokuwa kwa muda wa siku moja katika kila mwaka”.
Dk. Car katika maelezo yake aliongeza kuwa: “Vijidudu viambukizavyo maradhi huendelea na kunawiri maadam mwenye mwili anaendelea kula na kuvilisha, hivyo basi vitaendelea kukua na akijizuia kuwa vitadhoofika. Baadhi ya madaktari Waislamu na wasio Waislamu wameafiki shauri hili.
Pia Dk. Abdul Aziz bin Ismail anadai kwamba kufunga siku moja ni kinga ya maradhi kwa mwaka. Isitoshe kwa siku za hivi karibuni, kuna hospitali mbalimbali zinazohimiza na kusisitiza umuhimu huu, kadhalika mara nyingi tunashuhudia wagonjwa wengi ambao huzuiwa kula kwa manufaa ya afya zao.
Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Cairo, Dk. Muhammad Dhawahir, anasema: “Ugonjwa wa kuzidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment