Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Friday, April 24, 2009

Mario balotelli


Mario Balotelli
Ukata ulisababisha wazazi wake wamuuze
*Baada ya mafanikio wazazi wajitokeza kumdai
*Naye akawakataa kwa hasira ya kumuuza

UPO msemo wa kiswahili unasema kwamba ‘tajiri na mali zake masikini na watoto wake’ lakini msemo huu unaonekana kwenda kinyume kabisa na maisha halisi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Italia na klabu ya Inter Milan, Mario Balotelli Barwuah.

Historia ya mshambuliaji huyo wa InterMilan aliyezaliwa Agosti 12, 1990, imekuwa ya kusikitisha.

Balotelli amezaliwa nchini Italia katika mji wa Palermo, akiwa amezaliwa na wahamiaji kutoka Ghana ambao ni Thomas na Rose Barwuah.

Kutokana na hali ya wazazi wake kuwa ngumu kimaisha waliamua kuhama Palermo na kuhamia katika mji wa Mella, Brescia hii ilikuwa ni mwaka 1993, wakati huo Balotelli akiwa na umri wa miaka mitatu.

Wakiwa katika mji huo wazazi wake walijikuta wakikubali kumuuza kijana wao kisheria katika mahakama ya Brescia kwa famili ya Balotelli.

Wazee hawa hawakujua kama walikuwa wakiuza azina ambayo siku moja ingeweza kuwaondolea maisha yao ya dhiki na kulitangaza jina lao na kuwa kubwa duniani.

Kama ilivyo sheria za Italia Balotelli alisubiliwa kufikisha umri wa miaka 18 ili aombe uraia wa Italia, ambako alitambuliwa rasmi kama raia kisheria Agosti 13, 2008.

Baada ya wazazi wake waliomzaa wa familia ya Barwuah, kusikia kijana wao aliyekuwa tayari ameshaanza kuvuma na kuwa maarufu katika ulimwengu wa soka waliamua kujitokeza na kusema wao ndiyo wazazi wake halali.

Baada ya wazazi hao kutoa kauli hiyo Balotelli ambaye kisheria kwa wakati huo akitambuliwa kama mtu mzima naye aliwakana na kuwaambia kwamba “mzazi halali huwa hamuuzi mtoto wake, na hivyo mimi ni kijana halali wa familia ya Balotelli ambao wamemlea”.

Klabu alizochezea
Tangu akiwa kijana mdogo alikuwa ameshaonyesha kuwa atakuwa mchezaji hatari wa soka, kwani alipofikisha umri wa miaka 15, Balotelli alikuwa akikipiga kwenye klabu ya vijana ya Lumezzane, iliyokuwa ikipiga daraja la tatu la nchini Italia maarufu kama ‘Serie C1’.

Inter Milan
Haikumchukua muda mrefu kuonekana na klabu kubwa ya Inter Milan ambao walimsainisha kukipiga katika klabu hiyo kwa ndonge nono la pauni 340,000.

Kuchukuliwa kwa Balotelli na Inter Milan hakukuwa hivi hivi bali ni baada ya kuobnyesha uwezo mkubwa wa kukipiga vilivyo kwenye kikosi cha Taifa ya vijana chini ya miaka 17, inayojulikana kama Allievi Nazionali.

Pamoja na kuwa na miaka 16, lakini aliteuliwa kuwa mmoja ya wachezaji waliokuwa wakikipiga kwenye timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20.

Akiwa katika timu hiyo aliteuliwa na kuwa mchezaji nyota wa kikosi hicho. Kiwango chake kilikuwa na kushangaza hali iliyofanya amshawishi Mwenyekiti wa Inter Milan, Massimo Moratti kumsajili.

Desemba 16, 2007 Balotelli akicheza mechi yake ya kwanza Inter Milan akichukua nafasi ya David Suazo aliiwezesha klabu yake kuishinda klabu ya Cagliari kwa bao 2-0 katika Ligi kuu ya Italia ‘Seria A’.

Baada ya siku tatu kupita, alipangwa katika kikosi hicho akiwa ameanza katika mechi ya Coppa Italia dhidi ya klabu ya Reggina ambako alifanikiwa kupiga bao mbili kwa mguu wake katika mechi ambayo walishinda 4–1.

Januari 30, 2008 ‘SuperMario’ Balotelli aliifungia klabu yake bao mbili walipokutana na Juventus ambako aliiwezesha Milan kutinga robo fainali za Coppa Italia ambako walishinda 3–2.

Baoa lake la kwanza katika ligi kuu ya Italia ‘Seria A’ alilifunga Aprili 6, 2008 na kufanikiwa kushinda 2–0 dhidi ya Atalanta.

Wiki moja baadaye alifunga bao la pili la Ligi kuu walipokuwa wakicheza na Fiorentina na Mei 11, 2008, wakiwa nyumbani Siena, walitoka sare ya kufungana 2-2 na klabu ya Roma.

Katika wiki iliyofuata, Balotelli aliiwezesha klabu yake kuifunga Parma kwa bao 2-0.

Agosti 26, 2008 akicheza fainali za ‘Italia Supercup’ dhidi ya Roma, Balotelli aliingia katika kipindi cha pili akichukua nafasi ya Luís Figo, na kuwainua mashabiki wa klabu hiyo kwa kupiga bao katika dakika ya 83.

Katika mechi hiyo Inter ilitwaa ubingwa kwa kushinda 6-5 kwa penalti, baada ya mechi hiyo kuisha kwa kufungana 2-2.

Baaada ya kuisaidia klabu hiyo Balotelli alisainishwa mkataba mwingine wa miaka mitatu na Novemba 4, 2008, Balotelli aliendeleza upachikaji wake wa mabao ambako alipiga bao katika Ligi ya Mabingwa walipokutana na Anorthosis.

Katika Ligi hiyo Balotelli aliandika historia ya kuwa mchezaji mdogo kuweza kupachika goli katika ligi hiyo ambako alikuwa na umri wa miaka 18 na siku 85. (rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Obafemi Martins, aliyewahi kupachika akiwa na umri wa miaka 18 na siku 145).

Mechi zake za Kimataifa
Mechi za kimataifa alianza kucheza katika timu ya taifa ya vijana chinbi ya miaka 15 na chini ya miaka 17 , wakati huu wote alikuwa bado hajatambulika kisheria kama muitalia.

Agosti 7, 2007, siku tano kabla ya kufikisha miaka 17, aliitwa kwenye timu ya taifa ya Ghana na kocha, Claude Le Roy kwa ajili ya kukipiga mechi ya kirafiki na Senegal katika uwanja wa New Den Stadium huko London, England Agosti 21, 2007.

Baada ya kuitwa katika mechi hiyo Italia ilianza kujizatiti kwa ajili ya kuzuia kipaji chao ambako kocha wa timu ya taifa ya chini ya umri wa miaka 21, Pierluigi Casiraghi kutamka kwamba Balotelli ni raia wa halali wa Italia na hatakiwi kukipiga katika Timu ya taifa ya Ghana.

Agosti 13, 2008 alipewa uraia wa Italia ambao ulitangazwa katika mkutano wanahabari kuwa mchezaji huyo ni muitalia na ni mchezaji wa timu ya taifa ya Italia chini ya miaka 21 na Agosti 29, kocha wa timu ya vijana ya miaka 21 wa Italia, Casiraghi alimuunganisha kucheza katika kikosi kilichowakutanisha na timu ya Greece.

Katika mechi waliyokutana na timu ya Greece iliyo chini ya miaka 21 alipiga bao moja katika mechi waliyotoka sare ya 1-1, katika mechi iliyofuata aliipachikia bao mbili dhidi ya Israel na kuifanya ipate tiketi ya kucheza Euro 2009 chini ya miaka 21.


Tuzo alizopata
Trofeo Giacinto Facchetti (Under-20 Italian Championship) mwaka 2007
Torneo di Viareggio mwaka 2008
Serie A mwaka 2007-08.
Supercoppa Italiana 2008

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text