
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
IKIWA Julai 11 ndiyo siku ambayo Hispania ilifanikiwa kuandika historia ya kutwaa kombe la dunia lililofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika.
Pamoja na kwamba michuano hiyo ilikuwa kivutio lakini kuna wanamuziki ambao walioacha historia na kuweka historia kubwa ya kuwachanganya mashabiki waliokuwa amehudhuria hapo kulishuhudia kombe hilo.
Moja kati ya wasanii waliofanikiwa kung’aa kati ya 1,581 waliokuwa wanatoa shoo pale alikuwa mwimbaji Shakira toka Colombia, ambaye hakufikiriwa kama angeweza kufunika kutokana na waafrika wa nchini humo kupinga wimbo wake wa ‘Waka Waka’ (This Time for Afrika) kuwa utambulisho wa kombe la mwaka huu.
Mashabiki hao wakwenda mbali na kudai kuwa hawatamshabikia kwa kuwa Shakira ni mzungu hivyo wimbo huo ulitakiwa uandaliwe na mtu mweusi kwa kuiwakilisha Afrika.
Busara ya Shirikisho la Soka Afrika (Fifa), ilitumika na kuwaomba wamuache na walipomuacha aliishangaza dunia kwa ubunifu alioutumia wa kuishirikisha bendi ya kitamadunia ya Afrika kusini ya Freshlyground kwa kuimba wimbo wake wa ‘Wakawaka’.
Kwa kufanya hivyo alifanikiwa kuwakonga nyoyo zao hata wale waliokuwa wakimuombea mabaya ili aonekane hakuwa lolote.
Msanii mwingine aliyefanikiwa kufanya vema ni
Msanii kutoka Soweto, mjini hapa anayejulikana kama Stoan, Ladysmith Black Mambazo.
Wengine walioburudisha ni pamoja na waafrika kusini, TKZee, Mmarekani Black Eyed Peas, msanii wa Algeria Khaled, Osibisa wa Ghana na mwimbaji wa Hip hop, Pantsula.
Wimbo ambao ulifanikiwa kushika ni ‘Africa United’ uliimbwa kwa ushirikiano wa wasanii kama Jozi, Zulu boy wa Afrika Kusini, Silkour, 2 Face wa Nigeria, Kwesta, Chameleone kutoka Uganda, Awadi, Krotai na Samini kutoka Ghana.
Wengine ni Kubeka, Mafikizolo kutoka Afrika kusini walifanikiwa kuamsha kelele za hali ya juu kwa mashabiki hasa wa mjini hapa.
Mashabiki walipagawishwa na washindi wa Grammy, Ladysmith Black Mambazo ambao walishambulia jukwaa na kusababisha jukwaa la marais, Jacob Zuma na rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe kujikuta wakiinuka kwa furaha.
Si kwamba waimbaji hao waliwakosha mashabiki wa soka pekee bali hata mrembo wa kimataifa, Naomi Campbell, mcheza tenisi nyota, Rafael Nadal na mwigizaji wa Oscar, Morgan Freeman.
Pia waimbaji wa ngoma za kitamaduni za wenyeji Afrika kusini zilitumbiza na kufanikiwa kuwakamata kwa kutumia vifaa vya ushangiliaji maarufu kama vuvuzelas.
Msanii wa nyimbo za R&B, R Kelly (31), naye alifanikiwa kufunika vilivyo kama ambavyo ilitarajiwa.
Mwimbaji huyo ambaye ni mtayarishaji na mshindi wa tuzo kubwa za muziki za Grammys akiwakumbusha wimbo wake wa 'I Believe I Can Fly' na nyingine.
Naye Alicia Keys alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kukonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria onyesho hilo.
Alicia aliwachanganya mashabiki hao baada ya kuporomosha kibao chake cha kinachokwenda kwa jina la “No One”.
0 comments:
Post a Comment