WALIOKUWA wasanii mahiri wa kundi la East Coast Company (ECC), Ambwene Yesaya ‘AY’ na Khamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ wameungana na kutoa albamu ya pamoja itakayokuwa sokoni mwezi huu.
Akizungumza na Tanzania Daima hivi karibuni, jijini Dar es Salaam, mmoja wa wasanii hao, AY alisema kwamba tayari albamu imekamilika na itakuwa na nyimbo nane.
Alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwa kwenye albamu hiyo kuwa ni ‘Kula kwa Macho’ ambayo wamemshirikisha Talia, ‘Asubuhi’ ambao wameimba na Aboubakar Katwila ‘Q. Chief’, ‘Fungua Champagne’, ‘Nangoja Ageuke’, ‘Bounce’ au ‘Chameleone’ na ‘Umejuaje’ uliobeba jina la albamu.
Wasanii hawa hivi karibuni wameachia wimbo wao mpya unaojulikana kama ‘Asubuhi' waliomshirikisha ‘Q Chief’.
Akitoa sababu ya kufanya albamu ya pamoja, AY alisema kuwa wameamua kutoka na albamu hiyo kutokana na ushauri waliopewa na wasambazaji wa kazi za muziki.
Hivi karibuni, AY amepata tuzo ya Kisima ya wimbo bora wa Bongo Fleva kwa upande wa Tanzania, kupitia wimbo wake ‘Usijaribu’.
Historia za wasanii hawa zinatofautiana.
AY amezaliwa Julai 5, 1981 mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania, na kukulia Area C Dodoma, akiwa msanii anayetumia mtindo wa ‘Commercial’.
Baadhi ya albamu alizozitoa ni ‘Raha Kamili’ (mwaka 2003) na ‘Hisia Zangu’ aliyoitoa 2005.
Aliwahi kutamba na nyimbo zake kama ‘Mademu watafutaji’, ‘Usijaribu’, ‘Yule’ na nyinginezo nyingi.
AY ni mtoto wa tatu kati ya wanne wa familia ya marehemu, Allen Yessayah na mkewe Lydia Yessayah.
Alianza muziki mwaka 1996 akiwa na kundi lililojulikana kama S.O.G akiwa na wasanii wenzake kama, Benjamin Gamba ‘Buff G’ na Adam Semkiji ‘Snare’.
Mwaka 2002, AY aliamua kuitosa S.O.G na kuwa msanii wa kujitegemea na kuachia albamu yake ya kwanza iliyojulikana kama ‘Raha Kamili’ na kufuatiwa na ile ya ‘Hisia Zangu’.
Msanii huyu aliwahi kutoka na wimbo uliokuwa moto uliojulikana kama ‘Binadamu' uliokuwa ukizungumzia kuhusu watu wanavyomuheshimu mtu mwenye nacho na kumdharau asiye nacho.
Oktoba 2006, msanii huyo alitoka na wimbo mkali uliojulikana kama ‘Usijaribu’, ambao umejinyakulia tuzo mbili.
Kwa upande wa hapa nyumbani, wimbo huo umejinyakulia tuzo ya mwanamuziki bora wa Hip hop mwaka 2007 na hivi karibuni imejinyakulia tuzo ya Kisima nchini Kenya.
Katika historia ya muziki wa Bongo fleva, msanii huyo ndiye msanii wa kwanza kuchaguliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za Kora Afrika mwaka 2005.
Na mwaka huo huo, akichaguliwa kuwania tuzo za Kisima nchini Kenya kwa kupitia wimbo wake ‘Inategemea na mtu’.
Kwa upande wa Mwana Fa, yeye amezaliwa miaka 27 iliyopita jijini Tanga, na alianza kujishughulisha na mambo ya muziki mwaka 1993 wakati huo akiwa shule ya msingi jijini Tanga.
Mwana Fa alianzisha kundi lake lijulikanalo kama Crew Black Skin akiwa na wanafunzi wenzake kama Robilus na Getheerics mwaka 1995.
Mwaka 1998 aliingia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya masomo ya juu katika Sekondari ya Ununio Islamic High School, akiwa anachukua masomo ya Physics, Chemistry na Mathematics.
Baada ya kuhitimu mwaka 2000, alijiingiza katika mambo ya muziki ambapo mwaka 2003, alipata tuzo za Kili kwa kuwa mwanamuziki bora wa hip hop na wimbo wake ‘Alikufa Kwa Ngoma’.
Alibamu zake alizokwishatoa ni kama ‘Mwanafalsafa’ na ‘Toleo lijalo’ ambazo ziliwashika vilivyo wapenzi wa muziki.
Mwaka huu, alipewa tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana katika tuzo za Kili, ambayo aliifanya na Lady Jaydee.

0 comments:
Post a Comment