MWANAMUZIKI Rihanna ni mmoja kati ya wanamuziki wanatamba kwenye anga za muziki ambako hivi karibuni amejinyakulia tuzo mbili za MTV moja ikiwa ya Video ya mwaka na nyingine ya wimbo bora wa mwaka kwa kupitia wimbo wake wa "Umbrella".
Msanii huyo na Justine Timberlake ndio wasanii walioongoza kwa kujinyakulia tuzo nyingi zaidi kati ya wasanii waliokuwa wameingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Rihanna alikuwa na bifu na demu wa bosi wake rapa Jay Z, Beyonce Lowlence aliyekuwa akimtuhumu msanii huyo kuwa alikuwa anauhusiano wa kimapenzi na mchumba wake huyo.
Alikotoka mpaka umaarufu
Rihanna amezaliwa huko eneo la mtakatifu Michael, Barbados akiwa mtoto wa kwanza wa Ronald Fenty na mkewe Monica Fenty na kwa hivi sasa anaishi Diego, Califonia.
Msanii ambaye ni binti mkubwa katika familia yao yenye watoto watatu akiwa na wadogo zake wawili wa kiume, Rorrey na Rajad.
Msanii huyu ameanzia kusoma shule ya msingi ya Charles F. Broome Memorial iliyoko mjini Barbados, ambako baadaye alijiunga kwenye shule ya sekondari ya Combermere, ambapo aliunda kundi akiwa sambamba na wenzake wawili hata hivyo kundi hilo halikuweza kudumu sana.
Akiwa anasoma Sekondari hiyo alishiriki kwenye mashindano ya kumtafuta mlimbwende wa sekondari hiyo ambayo yakijulikana kama Miss Combermere ambayo yaliyofanyika mwaka 2004.
Mwanamuziki huyo alishinda na kuibuka kidedea kwenye mashindano hayo na baadae alitoa burudani katika shindano hilo, akiimba wimbo wa Mariah Carey uliojulikana kama "Hero".
Akionyesha nia ya dhamira yake ya kutaka kuwa muimbaji mwanadada huyo alipofikisha umri wa miaka 15, alimuomba rafiki yake kumtambulisha kwa mtayarishaji wa muziki, Evan Rogers, ambaye alikuwa na makazi yake huko mjini Barbados.
Rafiki yake huyo alimkubalia na kumpeleka na kwenda kumtambulisha kwa mtayarishaji huyo ambaye alikubali kumsaidia ambako walimtengenezea nyimbo na kuchukua nakala zake na kuzipeleka nchini Marekani kwa nia ya kumtafutia soko.
Nakala zake hizo zilichukuliwa na kupelekwa kwa rapa, Jay-Z, ambaye alikubali na kumsainisha kwenye lebo yake ya Def Jam Records.
Akiwa katika lebo ya Def Jam, Rihanna aliachia albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la ‘Music of the Sun’ ambayo aliiachia Agosti 30, 2005 ikiwa na nyimbo kali kali kama "Pon de Replay" ambayo aliiachia Oktoba 11, 2005.
Wimbo huo ulishika vilivyo ambako ilifikia kushika nafasi ya pili kwenye chati za nyimbo bora 100 za nchini Marekani za Billboard sambamba na chati za nchini Uingereza.
Wakati nyimbo zake zikiwa zinafanya viozuri albamu yake ilifanikiwa kuingia kwenye albamu 10 bora nchini Marekani na Canada, ambapo katika wiki ya kwanza ilifanikiwa kuuza jumla ya nakala 500,000 ambapo mauzo yake yalifikia platinum milioni 2 kwa duniani kote.
Wimbo wa pili aliouachia kwenye albamu yake ulikuwa ukijulikana kama "If It's Lovin' That You Want", haukuweza kufanya vizuri kwenye chati bora duniani za muziki.
Baada ya Def Jam kuona mafanikio aliyoyapata msanii huyo waliamua kumtolea albamu nyingine ya pili mapema.
Kete yake ya pili aliyoiachia ilikuwa ikijulikana kama ‘A Girl Like Me’ ambayo aliipeleka hewani mwaka 2006, ambapo katika mwaka huo alipata dili za kufanya matangazo na kampuni za Nike na J.C. Penney.
Albamu hii nayo ilifanikiwa kwani kwenye wiki ya kwanza tu, ilifanikiwa hadi kufikia nafasi ya tano katika chati za nchini Marekani na namba nne kwenye chati za Uingereza.
Katika albamu yake hiyo kutokana na ubora wa wimbo wake wa "SOS" ulisababisha Kampuni ya Nike kuutumia kwa ajili ya kutangaza bidhaa zao.
Wimbo huo ulifanikiwa kufikia hadi namba moja kwenye chati za nyimbo bora 100 za Billboard nchini Marekani, Uingereza, Australia.
Wimbo wake wa pili ulijulikana kama "Unfaithful" ambao aliandikiwa na muimbaji wa R&B anayekuja kwa kasi, Ne-Yo nao pia ulifanikiwa kushika vilivyo kwenye chati mbalimbali duniani kwa kukamata namba moja kwenye chati za nyimbo 10 bora.
Mwanadada huyu aliachia karata yake nyingine ya tatu kutoka kwenye albamu iliyokuwa ikijulikana kama "We Ride" lakini wimbo huo haukuweza kushika kwani ilishindwa kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali duniani.
Baada ya kuona muitikio wa wimbo huo wa tatu kwenda ndivyo sivyo mrembo huyo alisafisha njia kwa kuachia hewani wimbo wake wa nne uliokuwa kwenye albamu hiyo ulikuwa ukijulikana kama "Break It Off" aliomshirikisha mwana raga, Sean Paul aliyoitoa Februari 19, mwaka huu.
Baadhi ya nyimbo zake ambazo zimekuwa zikishika chati za nyimbo bora kali zinazochezwa kwenye kumbi za starehe duniani ni kama "Pon De Replay", "SOS", "Unfaithful", na "We Ride".
Rihanna aliachia pini lingine la kukata na shoka aliloandikiwa na msanii Ne-Yo lililojulikana kama "Just Be Happy" na baadae aliachia wimbo uliokuwa ukijulikana kama "Winning Women".
Mwaka huu ametoka na albamu ya kiukweli iliyojulikana kama ‘Good Girl Gone Bad’ ambayo aliiachia Juni 5, 2007 imekuwa gumzo nchini Marekani ambayo amewashirikisha Ne-Yo, Jay-Z na Timbaland.
Na wimbo wake wa kwanza wa kuitambulisha albamu hiyo ulijulikana kama "Umbrella" ambao aliutoa Machi 29, 2007 akiwa amemshirikisha rapa Jay Z.
Wimbo huu unapoteza isivyo kawaida kwani imekuwa ikishika namba moja kwenye chati bora duniani kwa hivi sasa una wiki 11.
Wimbo huu umeingia kwenye historia ya kukaa kwa muda mrefu katika chati za nyimbo bora duniani ambako kihistoria nyimbo ambazo zimewahi kukaa sana ni ya mwanamuziki Whitney Houston na wimbo "I Will Always Love You" ambayo ilikaa kwa wiki 10 mwaka 1992.
Katika albamu yake hiyo Rihanna ameachia wimbo wake wa pili unaojulikana kama "Shut Up and Drive" ambao nao unapoteza vilivyo kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni.
Wimbo wake mwingine unaochezwa zaidi kwenye kumbi za starehe ni "Don't Stop The Music" ambayo ameizindulia huko Canada.
Msanii huyo ameachia wimbo wake mwingine uliojulikana kama "Hate That I Love You" aliyoshirikiana na Ne-Yo, ambayo ameiachia Agosti 21, mwaka huu ambayo imefikia kushika namba sita.
Katika albamu hiyo Rihanna amefanya jumla ya kazi tatu na mtayarishaji Timbaland. pia ameshirikiana na msanii Justin Timberlake katika kuimba wimbo uliojulikana kama "Rehab".
Msanii huyo alikuwa na mahusiano na Josh Hartnett ambayo yalianza Oktoba 11, baada ya kukutana kwenye klabu ya NYC Pink Elephant kwenye tamasha la Nokia.
Lakini mapenzi yao yamevunjika bila kutoa sababu maalumu zaidi ya kusema kuwa yeye ni binadamu kama binadamu wengine kwa suala la kuachana ni la kibinafsi.
Julai 7, 2007, Rihanna alifanya onyesho la wazi mjini Tokyo, Japani ambalo lilikuwa likijulikana kama ‘Live Earth in Tokyo’.
Septemba 9, mwaka huu Rihanna ameshinda tuzo mbili za MTV moja ikiwa ya wimbo bora wa mwaka kwa kupitia wimbo wake wa ‘Umbrella’.
Pia msanii huyo ameshinda tuzo ya Video bora ya mwaka kwa kupitia wimbo wake huo wa "Umbrella".
Albamu yake ya mwaka huu mpaka sasa inashikilia namba 9 kwenye orodha ya albamu bora za mwaka huu.
Mwaka huu msanii huyo anashika vilivyo na albamu yake ya ‘Good Girl Gone Bad’ ambapo wimbo huo unaobeba jina la albamu unashikilia namba moja kwenye chati za nyimbo bora za nchini Marekani, Uingereza, Canada, Australia, Ujerumani na Ufaransa.
Mwisho.

0 comments:
Post a Comment