Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, May 10, 2009

mbabe wa Filipino


Manny Pacquiao
Bingwa anayewaniwa na Mayweather Jr.
*Ni baada ya kuuangusha mwamba Rick Hatton
*Bingwa mara nne wa kwanza Asia, Filipino


BAADA ya bondia, Manny Pacquiao wa Philippines, kumsimamisha kwa KO raundi ya pili Ricky Hatton wa England na kutwaa ubingwa wa dunia wa Welterweight.

Pambano hilo la aina yake lilianza kwa Pacquiao kudhihirisha kuwa si bondia wa kuchezea baada ya kumpa konde la kushoto mpinzani wake lililompeleka sakafuni sekunde chache baada ya pambano kuanza.

Akitoka kumchapa Oscar De La Hoya, Pacquiao alimdhibiti Hatton na kumpeleka sakafuni mara mbili kabla ya kumkalisha mara ya tatu ambayo hakuinuka hadi mwamuzi Kenny Bayless alipomaliza pambano dakika 2:59 ya raundi ya pili.

Swali ambalo bado linaumiza kichwa wapenzi wa ngumi ni kwamba Pacquiao atauweza muziki wa Mayweather Jr. mwezi julai? Baada ya kushinda pambano hilo.

Mbabe huyo ambaye mwaka huu ametajwa na jarida la Time Magazine kuwa mmoja ya watu walio na mvuto mwaka 2009.

Kihistoria bondia huyu amezaliwa nchini Ufilipino Desemba 17, 1978, akipewa jina la Manny ‘Pac-Man’ Pacquiao.

Mbabe ambaye ni bingwa wa dunia wa WBC katika uzani wa lightweight, WBC super featherweight, IBF super bantamweight na WBC flyweight.

Mwamba huyu amekuwa raia wa kwanza kutoka Ufilipino na bara la Asia kushinda jumla ya mataji matano tofauti makubwa duniani.

Pacquiao ambaye amezaliwa Kibawe, Bukidnon, Mindanao kwa sasa akiwa anaishi katika jiji la Santos, South Cotabato, Ufilipino anaishi na mkewe anayejulikana, Jinkee Pacquiao, na wamebahatika kupata watoto wanne.

Pacquiao ni mchezaji mzuri wa ngumi na hakuibuka katika nyakati hizi kama wengi wanavyofikiria.

Mchezaji huyu ameanza kucheza ngumi za kulipwa akiwa na umri wa miaka 16 pekee.

Na mchezo wake wa kwanza alioanza kucheza kama mchezaji wa kulipwa ulikuwa ni kati yake na Edmund ‘Enting’ Ignacio aliocheza Januari 22, 1995 na alifanikiwa kushinda kwa pointi.

Baada ya kushinda mchezo huo aliongeza uzito waike kutoka 106 1bs na kuwa 113 lbs na hii ni baada ya kushindwa pambano lake na Rustico Torrecampo katika raundi ya tatu kwa (KO).

Bingwa huyo alifanikiwa kutwaa ubingwa wa WBC katika uzani wa Flyweight baada ya kumtwanga Chatchai Sasakul katika raundi ya nane lakini mkanda huo aliupoteza kwa Medgoen Singsurat wa Thailand.

Baada ya kushindwa na Singsurat, Pacquiao aliongeza uzito na kuwa 122 lbs sawa na kilogramu 55 na kuhamia Super bantamweight, ambako alifanikiwa kutwaa mkanda wa WBC katika uzani huo wa Super Bantamweight.

Pacquiao alifanikiwa kutwaa ubingwa wa IBF Super Bantamweight dhidi ya Lehlohonolo Ledwaba, aliyemtwangwa kwa TKO, Juni 23, 2001.

Lakini bondia huyu alijikuta akitoka sare katika pambano la raundi sita dhidi ya Agapito Sanchez.

Pamoja na kwamba pambano lake na Marco Antonio Barrera halikuwa la ubingwa ila lilisababisha jina lake kuwa juu.

Pambano hilo lilimfanya aongeze uzito wake akipania kucheza pambano lake la kwanza la featherweight, na alifanikiwa kumpiga Barrera kwa TKO ya raundi ya 11 katika pambano lililochezwa ukumbi wa Alamodome, San Antonio, Texas.

Miezi sita baada ya kucheza na Barrera, Pacquiao alicheza dhidi ya Mexico, Juan Manuel Márquez, na kutwaa ubingwa wa duniani wa WBA na IBF katika uzani wa Featherweight.

Pambano hilo lilimalizika kwa majaji wote watatu kuwapatia pointi 10-7 na kulifanya pambano hilo kuwa sare.

Baada ya kutoka sare alitafutiwa mbabe mwingine toka Mexico, Érik Morales katika pambano lililofanyika Machi 19, 2005, katika ukumbi wa MGM Grand, katika pambano hilo, Pacquiao alijikuta akipoteza kwa pointi.

Septemba 10, 2005, Manny Pacquiao alimtoa kwa ‘KO’, Héctor Velázquez, na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa WBC International Super Featherweight.

Baada ya kushinda alipewa pambano jingine la maruadiano kati yake na Morales, katika pambano lililokuwa la raundi 10 alishinda kwa ‘KO’.

Julai 2, 2006, Pacquiao akicheza dhidi ya Oscar Larios, aliyekuwa bingwa mara mbili wa super bantamweight. Katika pambano hilo Pacquiao alimshinda Larios na kutetea ubingwa wake wa WBC International Super Featherweight. katika pambano lao la marudiano aliendeleza kichapo kwa kumtoa kwa ‘KO’ ya raundi ya pili.

Mwishoni mwa mwaka 2006, alitajwa na Chama cha HBO kama piganaji mwenye mvuto wa mwaka ikiwa ni pamoja na jarida la Ring likimtaja kuwa mpambanaji wa mwaka.

Juni 29, 2007, akitajwa kama mpiganaji bora namba moja alifanikiwa kumpiga Marco Antonio Barrera. Katika mchezo wake wa marudiano pia alishinda mchezo huo.

Katika pambano lake la marudiano na Barrera, Pacquiao alifanikiwa kuingiza dola milioni 5.

Pacquiao ndiye bondia anayetajwa kushikilia nafasi ya pili kwa sasa kwa ubora ukimuondoa Floyd Mayweather Jr.

Machi 15, 2008 akicheza pambano la marudiano dhidi ya Juan Manuel Márquez alifanikiwa kumtoa kwa ‘KO’ na kushinda ubingwa wa WBC na kuweka historia ya kuwa mfilipino wa kwanza kushinda mataji matatu makubwa duniani katika uzani tofauti.

Mwaka 2008, alikutana na mabondia kama David Díaz na kumtoa kwa ‘KO’ ya raundi ya nane na kutwaa ubingwa wa WBC lightweight na kuwa taji la nne.

Akiwa ni bingwa wa WBA, WBC, WBO na IBF katika uzani wa lightweight, alicheza na David Diaz na kujiingizia kiasi cha dola milioni 12.5, Pacquiao alifanikiwa kushinda kwa ‘KO’.

Katika pambano lake na De La Hoya
La Desemba 6, 2008, Pacquiao alifanikiwa kumchapa kwa ‘TKO’.

Baada ya kutembeza kipigo hicho mbabe huyo alipangwa kucheza na Ricky Hatton katika pambano lililochezwa Mei 2, 2009, alifanikiwa kuandika historia nyingine hapa kwa kumpiga kwa ‘KO’ ya raundi ya pili.

Pacquiao ni mwanasiasa mzuri kwani amewahi kuwania ubunge wa jimbo la South Cotabato la nchini kwao Ufilipino, ila alishindwa na Darlene Antonino-Custodio aliyepata kura 139,061 na yeye aliambulia 75,908.

Pacquiao ameahidi kurejea tena katika siasa mara baada ya kustaafu mchezo wa ngumi.

Pia mwanamasumbwi huyo ni muigizaji wa filamu baada ya mwaka huu kutoa filamu inayozungumzia maisha yake ameamua kuachia filamu inayohusu maisha yake.

Yupo mbioni kutoa filamu nyingine aliyopanga kuitoa na muigizaji maarufu, Sylvester Stallone ‘Rambo’ kutengeneza filamu ya pamoja hivi karibuni.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text