Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, May 10, 2009

Mbabe wa kike


Maryse Ouellet
Mwanamieleka aliyeitosa fani ya mitindo
*Ndiye bingwa WWE kwa wanawake

KWA wapenzi wa mchezo wa mieleka hasa wa Chama cha Mieleka Dunaini (WWE), wamekuwa na hisia kwamba huenda mchezo huu unachezwa na wanaume pekee.

Aliyefanya leo katika safu hii tumuandike mchezaji mwanamke ni msomaji wetu anayejulikana kwa jina la Kassim Khamis wa Mwanza aliyeuliza swali kuwa kwa nini wanawake hawachezi mchezo huu?

Nikamjibu kuwa wanawake wanacheza kama wanavyocheza wanaume na kwa kuanzia nikamwambia leo nitamuweka bingwa wa WWE kwa upande wa wanawake.

Bingwa huyo anakwenda kwa jina la Maryse Ouellet aliyezaliwa Januari 21, 1983, aliye na asili ya Ufaransa na Canada.

Historia ya bingwa huyu ni ya kushangaza kwani kabla ya kujiunga na mchezo huu alikuwa akijihusisha na shughuli za uanamitindo.

Inadaiwa kwamba kwa mara ya kwanza kutangaza kujiunga na mchezo huu wengi walimshangaa kwa uamuzi wake wa kuacha kuendelea na mitindo na badala yake kuamua kwenda kucheza mchezo utakao uharibu uzuri wake ikiwa ni pamoja na kuhataraisha maisha yake.

Mwanamieleka huyo aliwaondoa shaka na kuwaambia kwamba anaamini anauweza mchezo huo ambao amekuwa akiuhusudu kwa muda.

Kwa kuonyesha alikuwa anajiamini kwa kile alichowaambia hivi sasa mwanadada huyu ndiye bingwa wa WWE.

Maryse ambaye ana urefu wa futi 5 na nchi 8, na uzito wa kilogramu 57, anasema kwa sasa hafikirii kuuacha mchezo huo.

Rekodi yaMaryse Ouellet katika mitindo ilikuwa nzuri kutokana na sababu ya uzuri wake.

Mwanadada huyu mwaka 2003 amewahi kushinda na kuwa Miss Hawaiian katika ukanda wa Canada.

Baada ya kumaliza muda wake mwaka 2004 alianza kufanya matangazo katika majarida ya urembo, magazeti na televisheni za Canada, pia sura yake imewahi kupamba kurasa ya jarida maarufu la warembo la Playboy mwaka 2006.

Baada ya kutoka katika jarida hilo mwaka 2006, ndipo Maryse aliamua kujiingiza moja kwa moja katika mchezo wa kulipwa kati9ka chama cha WWE.

Mwanadada huyo hakuingia moja kwa moja katika mashindano hayo bali alishiriki katika mashindano ya kuwatafuta wababe yanayojulikana kama ‘Diva search’ katika mashindano hayo alimaliza kwa kuingia katika wachezaji nane bora.

Akiwa mchezaji wa WWE Julai 4 akicheza katika mashindano makubwa ya ‘Raw’ ambayo huwashirikisha wababe kibao alifanikiwa kukamata nafasi ya pili.

Yalipomalizika mashindano hayo Agosti 13–17, 2006 alipelekwa kuwania mkanda wa Ohio Valley Wrestling (OVW) ambao unatambuliwa na WWE.

Agosti 24, 2006 alisainishwa na WWE kucheza OVW kwa ajili ya kucheza zaidi.

Desemba 16, 2006 akiwa katika mashindano ya ‘house show’ yaliyofanyika Kentucky akiwa na timu yake ya akina Katie Lea, Kelly Kelly, She Nay Nay na Victoria Crawford walifanikiwa kuwachakaza wababe ODB, Milena Roucka, Josie, Beth Phoenix na Melody.

Machi 2007, alifanikiwa kutwaa ubingwa wa OVW akimchapa Melody.

Aprili 2007 akiwa chini ya umeneja wa Sylvain Grenier, Maryse alifanikiwa kutwaa ubingwa wa uzito wa juu wa FCW Southern.

Oktoba 2007, Maryse kwenye mashindano ya WWE ya nchi za Ulaya akiwa na Michelle McCool walifanikiwa kuishinda timu ya akina Victoria na Katie Lea.

Machi 7, 2008 akiwa katika mashindano ya SmackDown, Maryse alifanikiwa kuwapiga wababe kama Victoria, Michelle McCool, Cherry, na Eve Torres.

Machi 28, 2008 Maryse akiwa na Victoria walifanikiwa kuiangusha timu ya Cherry na McCool.

Katika pambano la ‘SmackDown’ Mei 16, 2008 alijikuta akipoteza dhidi ya Cherry.

Baada ya wiki mbili ya kipigo, Maryse akiwa na Victoria na Natalya walifanikiwa kutembeza kipigo kwa timu ya akina Cherry, Michelle McCool na Maria.

Baada ya kushinda pambano hilo, Maryse aliishia kuuguza maumivu ya pua aliyoyapata kutoka kwa kipigo cha Maria.

Septemba 23, 2008, Maryse akirejea katika hali yake ya kawaida alitembeza kipigo kwa McCool katika pambano lisilokuwa la ubingwa.

Desemba 19, 2008 Maryse alifanikiwa kumtembezea kipigo Maria.

Baada ya kutembeza kipigo hicho aliendeleza kipigo kwa Michelle McCool na kuwa bingwa mpya wa Divas.

Desemba 28, 2008 akiwa katika mashindano ya ‘house show’ huko North Carolina, Maryse alipata majeraha ya kifundo cha mguu alipokuwa akicheza dhidi ya timu ya The Bella Twins.

Januari 23, 2009 alirejea na nguvu mpya na timu yake ya tag akiwa na Michelle McCool waliwakunja Maria na Eve Torres.

Aprili 5, Maryse alijikuta akiangukia pua katika mashindano ya WrestleMania XXV, baada ya Santino Marella kumtembezea kipigo na kuibuka mshindi.

Aprili 13, 2009 Maryse alifanikiwa kutwaa ubingwa wa WWE katika mashindano ya Raw brand.

Nje ya ulingo
Nje ya ulingo, Maryse ni msoni wa aliye na shahada ya Biashara na utawala na pia ana mkanda mweusi wa ‘martial arts’.

Aprili 2007, Maryse alikuwa mmoja kati ya watu walioigiza kwenye video ya muziki ya msanii Timbaland ya ‘Throw It On Me’.

Ubingwa alizotwaa
1. Bingwa wa Chama cha Mieleka (WWE)
2. Bingwa wa mashindano ya WWE Divas Championship
Mwisho.

1 comments:

Shabani Matutu said...

blogg yako bomba lakini unachelewesha kuweka makala kibao

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text