Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Friday, May 15, 2009

wa leo mieleka

Mbabe anajishughulisha na muziki
*Ndiye baba wa mbabe Randy Orton
*Randy anapozidiwa huingia kumsaidia

UNAPOZUNGUMZIA mchezo wa mieleka ni vigumu sana kuwakuta wachezaji ambao wametokea kucheza mchezo huu pasipo wazazi wao kucheza mchezo huu.

Kutokana na historia hiyo huwezi kukosea iwapo ukisema mchezo huu ni wa ukoo.

Leo katika safu yetu hii tunamzungumzia mbambe Bob Orton Jr ‘Cow boy’ mzazi wake na mbabe, Randy Orton.

Mbabe huyo anauzito wa futi 6 na nchi 1 na uzito wa kilogramu 110 kg, akiwa amezaliwa Novemba 10, 1950 .

Jina halisi la mbabe huyo ni Robert Keith Orton, Jr. akiwa amezaliwa Novemba 10, 1950, ambaye alikuwa akitumia jina la "Cowboy" Bob Orton pindi awapo jukwaani
Katika ukoo wa mzee huyo baadhi ya watu waliopita na wanaocheza mchezo huu ni mwanaye Randy Orton, baba yake anayejulikana kama Bob Orton, Sr. na kaka yake na Barry O.

Kwa mara ya kwanza mbabe huyo alijiingiza kwenye mchezo huo mwaka 1972 akiwa maeneo ya Florida na Georgia na wakati mwingine akiwa alikuwa akicheza akiwa amevaa kinyago na wakati huo akitumia jina la ‘Young Mr. Wrestling’.

Mbabe huyu alianza kucheza katika timu aliyokuwa akiiunda na baba yake aliyekuwa akijulikana kama, Bob Orton Sr.

Mwaka 1980 aliachana na baba yake na kujiunga na chama cha NWA akiwa na mpiganaji mwenzake waliounda timu moja aliyejulikana kama, Don Kernodle.

Akiwa na mbabe mwenzake huyo walifanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia wa Tag unaotambuliwa na NWA.

Kutokana na ubora wake Orton Jr aliahidiwa kupewa kiasi cha dola 25,000 kama ofa na kamisheni ya mieleka ya NWA .

Mwaka 1983 Orton Jr akicheza na mbabe Ric Flair alifanikiwa kumpiga mpaka kumtegua shingo.

Kutokana na kumuumiza huko kulimfanya Flair kutamka kwa mara ya kwanza kutangaza kutangaza kustaafu.

Mwaka 1984, Orton Jr alijiunga na Chama cha mieleka cha WWF kwa sasa WWE ambako alianza kutumia jina la ‘Ace’.

Mechi kali aliyocheza akiwa WWF ilikuwa dhiodi ya Jimmy Snuka aliyocheza mwaka 1985 na kufanikiwa kushinda.

Aliposhinda mechi hiyo alifanikiwa kupata mashabiki zaidi.

Mei 11, 1985, Orton Jr alijikuta akichezea kichapo kutoka kwa bingwa wa wakati huo wa WWF, Hulk Hogan.

Mwaka 1986 akicheza pambano dhidi ya Mr. T katika mashindano ya WrestleMania 2 ambako alifanikiwa kushinda mechi hiyo iliyokuwa na tambo kutoka kila kona.

Akiwa katika mshindano ya WrestleMania III, alifanikiwa kuliweka juu jina lake kwa kushinda mechi kibao mwaka 1987.

Orton Jr alikihama tena chama cha NWA mwaka 1989 na mwaka 1999 alitangaza kustaafu lakini mwaka 2000 alitangaza kurejea tena.

Novemba 2004, akiwa na akina Todd Hanson na Beau Douglas waliishinda timu ya akina Kamala na Gino Marktino.

Baada ya kushinda pamnbano hilo, Februari 3, 2005, Bob Orton Jr alitunukiwa tuzo ya heshima ya mbabe wa jumla.

Kwa kuonyesha kuwa tuzo hiyo alipewa kihalali wiki iliyofuta ya kutunukiwa tuzo hiyo aliingia kwenye mashindano ya WrestleMania 21, akiwa na kijana wake Randy Orton alimsaidia kumsambaratisha The Undertaker.

Alionekana tena katika mashindano ya WrestleMania, baada ya kumuona mwanaye anazidiwa na The Undertaker .

Katika mechi hiyo walifanikiwa kumuingiza The Undertaker kwenye jeneza.

Agosti 21, 2005, aliingilia pambano lililokuwa kati ya Randy na The Undertaker ambako Randy alifanikiwa kushinda pambano hilo.

Orton akiingia na mwanaye Randy katika pambano la ‘No Mercy’ Oktoba 9, 2005, walifanikiwa kumshinda mbabe The Undertaker na kumuingiza kwenye jeneza.

Desemba 16, 2005 katika pambano la SmackDown!, Orton Jr akiwa peke yake alijikuta akichezea kichapo kutoka kwa mbabe The Undertaker.

Katika mashindano yaliyofanyika Armageddon mwaka 2005, Orton Jr akiwa na mwanaye Randy Orton walifanikiwa kumuingiza kwenye jeneza The Undertaker.

Februari 13, 2006, Orton alitangaza kustaafu mchezo huo.

Kwa sasa Orton Jr anajishughulisha na utangazaji na shughuli za umiliki wa chama chake cha mieleka cha Tennessee Mountain Wrestling cha huko Knoxville, Tennessee.

Maisha yake ya kawaida mbabe Orton Jr anaishi na mkewe, Elaine Orton, ambaye ni nesi wa hospitali ya Christian Hospital NE ya Missouri.

Mama huyo wamebahatika kuzaa naye watoto watatu ambao ni Randy, Rebekah na Nathan.

Kwa sasa Orton Jr anaye mjukuu wa kike, Alanna Marie Orton, ambaye ni binti wa kijana wake Randy Orton aliyezaa na mkewe, Samantha.

Kwa sasa Orton Jr anaishi Florissant, Missouri na anasema kwamba mchezo ambao anauzimia ni mieleka hata akiwa nyumbani huwa anakwenda kwenye majumba ya mazoezi ikiwa ni pamoja na shughuli za uimbaji wa muziki.

Mwisho.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text