MOJA ya sifa kubwa ya mchezaji Jeff Hardy ni miruko anayokuwa akiruka kutoka katika umbali mrefu pindi anapokuwa amemuangusha mwanamieleka mwenzake na kumuangukia juu ya mgongo wake.
Kutokana na tabia yake hiyo imemsababishia mbabe huyo mwaka jana kulazwa kwa kuvunjika mgongo wake.
Mbabe huyo ambaye jina lake kamili ni Jeffrey ‘Jeff’ Nero Hardy akiwa amezaliwa Agosti 31, 1977 akiwa na urefu wa futi 6 na inchi moja na uzito wa kilogramu 102 akiwa amezaliwa huko Cameron, North Carolina.
Historia ya mbabe huyu haikuanzia katika mashindano ya WWE bali alianzia kwenye mapambano ya Organization of Modern Extreme Grappling Arts (OMEGA) akiwa na kaka yake Matt Hardy.
Baada ya kusaini katika chama cha WWE alimshawishi kaka yake Matt kuondoka naye na kuanzisha timu moja iliyokuwa ikienda kwa jina la Team Xtreme.
Akiwa katika timu hiyo na kaka yake, walifanikiwa kutwaa ubingwa mara sita wa Tag na bingwa mara moja wa Tag wa WCW.
Akiwa peke yake ameshatwaa ubingwa mara tatu wa WWE na bingwa mara mbili wa uzito wa juu, bingwa mara nne wa mabara, bingwa mara moja wa uzito wa juu wa Light na bingwa mara moja wa Ulaya.
Pia alitwaa ubingwa mara tatu wa Hardcore. Ukiachilia mieleka mbabe huyu pia hujihusisha na
Muziki, upakaji wa rangi na uchoraji wa katuni.
Kihistoria Hardy, tangu alipokuwa kinda alikuwa akivutiwa na mchezo huu na alijikuta akianza kucheza mchezo huu kimataifa akiwa na miaka 16 pekee.
Na mechi yake ya kwanza akiwa na ACW akicheza dhidi ya Razor Ramon, Mei 24, 1994 wakati huo akiwa anafanya kazi bila kuajiliwa ila akiwa analipwa kwa kazi anayoifanya.
Kabla ya Jeff Hardy kujiingiza kwenye Chama cha WWF alikuwa akitengeneza mihuri, kuchora katuni na paka rangi, kaka yake Matt alikuwa akicheza katika mapambano ya OMEGA akiwa na Thomas Simpson na baadaye alianza kucheza na Jeff kwenye kundi hilo.
Baada ya kuwa pamoja kwenye chama cha WWF katika kundi hilo la OMEGA Jeff alimshauri mwenzake kubadili jina ambako mwaka 1998, wakiwa chini ya ukufunzi wa Dory Funk, Jr. pamoja na wanamieleka wenzao Funkin' Dojo, Kurt Angle, Christian, Test na A-Train.
Wababe hawa walijiita Hardy Boyz, na mwaka 1999, walimuongeza Michael Hayes akawa kama Meneja wao.
Julai 5, 1999 walifanikiwa kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa Tag wa WWF baada ya kuisambaratisha kambi ya Acolytes lakini baada ya mwezi mmoja walijikuta wakipoteza kwa kundi hilo taji hilo.
Oktoba 17, 1999 wakiwa katika mapambano ya No Mercy, Hardy Boyz walishinda taji la Tag la WWF likiwa taji lao la kwanza la mashindano ya ngazi dhidi ya akina Edge na Christian.
Mwaka 2000, Hardy Boyz walipata meneja mwingine aliyejulikana kama Lita na Meneja huyo alisababisha wabadili jina lao na kujiita Team Xtreme.
Baada ya kutoa kipigo kwa akina Edge na Christian mwaka 2000 walitangaza vita ya kutaka kurudiana na timu hiyo ambako katika mechi ya marudiano walifanikiwa kutetea taji lao la WWF kwa mara nyingine.
Katika mapambano ya SummerSlam, kundi hilo likicheza katika mapambano ya meza, ngazi na viti maarufu kama (TLC), walifanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kuwachakaza akina Dudley Boyz, Edge na Christian.
Mwaka 2001, Hardy alifanikiwa kutwaa taji la ubingwa la WWF akiwa peke yake alipocheza dhidi ya Triple H.
Aliendelea kufanya mambo makubwa kwani mwaka huo alifanikiwa kutwaa ubingwa wa uzito wa juu wa Light dhidi ya Jerry Lynn.
Kwa kuonyesha kuwa hakuwa kijana wa mchezo mwaka huo akicheza dhidi ya Mike Awesome alifanikiwa kumchapa na kutwaa ubingwa wa Hardcore.
Mwishoni mwa mwaka 2001, akicheza katika pambano la Vengence dhidi ya kaka yake, Matt aliweza kumuadhibu katika pambano hilo ambalo halikuwa la ubingwa.
Mwaka huo 2001 akicheza dhidi ya mbabe The Undertaker alishindwa kutetea ubingwa wake wa Hardcore na kukubali kupokea kipigo toka kwa mbabe huyo.
Baada ya kupokea kipigo hicho alikaa nje ya ulingo kwa muda akitibia maumivu ya mgongo na Julai 2002, Hardy alirejea ulingoni na nguvu mpya na kufanikiwa kutwaa ubingwa wake wa tatu wa Hardcore dhidi ya Bradshaw.
Mwaka 2003 alitwaa ubingwa wa ulaya baada ya kumuadabisha William Regal, lakini alipoteza taji hilo kwa Rob Van Dam.
Mwaka 2005 akiwa TNA alifanikiwa kutwaa taji hilo kwa kumchakaza mbabe, A.J. Styles. Kutokana na uwezo wake NWA waliamua kumtuza taji la uzito wa juu kwa kuwa mchezaji bora.
Septemba 8, 2005 alipoteza taji lake kwa Jeff Jarrett, lakini Oktoba 2005, alilirejesha taji hilo na alilipoteza February 2006, Hardy alipoteza ubingwa wake wa NWA kwa Abyss.
Mwaka 2008 akimtwanga Umaga, alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mabara wa WWE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment