Sayari mpya yagunduliwa
*Inatembea bila kufuata ‘Orbit’
LONDON, England
IMEPITA miaka mingi sasa tangu wanasayansi wagundue uwepo wa sayari tisa ambazo ni Mercury, Venus, Earth, Mars, Saturne, Jupiter, Uranus, Neptune na Pluto haijawahi kutokea uchunguzi mwingine mpya lakini hivi karibuni wanasayansi wa uingereza wakishirikiana na wenzao wa Geneva wamedai kugundua uwepo wa sayari nyingine mpya.
Moja ya maajabu yaliyogunduliwa na wanasayansi hao yanayoonekana katioka sayari hiyo ni kuzungunguka kwake katika njia ya orbit sawa na nyota nyingine zinavyozunguka.
Pamoja na kuzunguka kama ilivyo kwa sayari nyingine lakini yenyewe imekuwa tofauti kwa kuwa inazunguka katiika njia isiyokuwa sahihi, pia pindi inapokuwa inazunguka inakuwa nyuma ya mlundikano wa nyota.
Inakadiriwa kuwa mwanga unaotolewa na sayari hiyo ni sawa na mianga ya miaka 1,000 iliyopita.
Pamoja na kwamba watafiti hao walifanya siri kwa kutotangaza kwa wanahabari lakini siri hiyo ilitolewa na mwanasayansi mmoja anayejulikana kama Sara Seager.
Akitoa taarifa hiyo, mwanasayansi huyo alisema “Pamoja na kwamba kundi la wachunguzi hawa hawakutaka kusema mbele ya wanahabari kuhusu ugunduzi wao lakini ukweli ni kwamba wanasayansi hawa wamegundua uwepo wa sayari hiyo mpya ya nyongeza,”.
Inasemekana kwamba ssayari hiyo pindi inapokuwa katika safari zake inakuwa inakuwa na mwanga mkali huku ikiacha vumbi. Mwendo wa sayari hiyo husababisha kuacha lundo la mawingu mahali inapokuwa imepenyeza, huku ikiwa imetengeneza mzunguko unaokuwa na mwanga kama moto.
Kundi hilo la wanasayansi wa WASP na wengine wanakadiria inaweza ikawa moja ya sayari kubwa katika historia ya sayari.
Katika maelezo yake Seager alisema kuwa “Nadhani sayari hii itakuwa na muonekano mzuri zaidi, ikiwa ni pamoja na kuvutia kuliko sayari ambazo zimekuwapo kwa muda, na hii ni nadharia tu, lakini itakuwa nzuri zaidi pindi itakapohakikishwa."
Wanasayansi wanafikiria kwamba eneo la Sayari hiyo inapopita si la kudumu bali linakuwa linabadilika mara kwa mara kutokana na ukubwa wa sayari yenyewe.
Kuna habari kuwa mapema wiki hii Taasisis ya Uchunguzi wa Masuala ya Sayansi wa nchini Marekani (NASA), wamesema kwamba watafanya utafiti wa kutafuta ukweli kama ipo sayari hiyo.
Katika uchunguzi wa WASP imegundulika kwamba sayari hiyo ni kubwa ikiizidi kwa mara mbili ile sayari kubwa kuliko zote kwa sasa inayojulikana kwa jina la Jupiter.
Imedaiwa kwamba iwapo NASA watakubaliana na uchunguzi huo inaweza ikatangazwa kuwa sayari kubwa kuliko zote na pia itakuwa imeongeza idadi ya sayari kutoka tisa na kuwa 10.
Akiendelea kuelezea kuhusu uvumbuzi huo mwanasayansi Seager alisema kuwa sayari hiyo inaongeza nguvu yake kutoka ndani ikiwa ni pamoja na kutengeneza misuguano yenyewe ambayo hutengeneza nguvu na kuifanya kuwa kubwa,”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment