
Bangi husababisha magonjwa ya Ini, Figo na akili
*Awali ilidhaniwa kupunguza msongo
*Calfornia, New Mexico, Canada waitumia kama dawa
BAADA ya kukuwepo kwa baadhi ya tafiti zilizokuwa zikiruhusu uvutaji wa bangi kwa madai kuwa ilikuwa ikiwasaidia wagonjwa hasa waliokuwa wakisumbuliwa na msongo wa mawazo imesababisha baadhi ya nchi kuruhusu matumizi yake.
Pamoja na kwamba mawazo ya wengi yalikuwa yakifikiria nchi ya Jamaica ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kwa watumiaji wengi ingekuwa ya kwanza kuruhusu lakini ukweli ni kwamba nchi ya Canada ndiyo ilikuwa ya kwanza kukubali bangi kutumiwa kama dawa ya maradhi.
Baada ya utafiti huo wa awali hivi karibuni watafiti wengine wamegundua kuwa matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasababisha kujiongezea madhara badala ya kutibu kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.
Watafiti hao wamekwenda kinyume na wale wa kwanza kwa kusema kuwa matumizi yake yanauwezekano mkubwa wa kumletea mtumiaji magonjwa ya kupunguza uzito mara kwa mara, magonjwa ya Figo na Ini na ugonjwa wa akili.
Watafiti waliogundua athari hizo ni wale wanaotokea nchini, Australia ambao katika utafiti wao wamegundua kuwa zaidi ya vijana wanaofikia 3,100 walio katika umri wa miaka 20 ndio wamekuwa watumiaji wakubwa wa bangi.
Utafiti wao umekwenda mbali na kubaini kwamba asilimia 18 ya vijana hao ni wale waliojiingiza katika matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa muda wa miaka miwili au mitatu.
Asilimia nyingine 16 ya vijana wa umri huo wamebainika kutumia kwa muda wa kati ya miaka minne hadi mitano.
65 kati ya watumiaji wamegundulika wameshaathirika na maradhi ya ugonjwa wa akili.
Wakati hao wakisumbuliwa na tatizo hilo wengine 233 wamebainika kuathirika na figo na Ini.
Watafiti hao pia wamebaini vijana wengine kati yao wamesumbuliwa na tatizo la kupata uchizi (wehu).
Baada ya kubaini hayo watafiti hao wametoa ushauri kwa vijana kutotumia dawa hizi za kulevya kwa vijana kwa zaidi ya miaka sita au zaidi tangu pale siku ya kwanza alipoanza kutumia.
Watafiti hao wanasema kuwa kwa wale ambao sasa wamevuta kwa muda mrefu kati ya miaka 15 na zaidi wengi wao wamekumbwa na tatizo la kiakili.
Kwa mujibu wa Dk. John McGrath, wa kituo cha uchungunguzi wa Afya ya wagonjwa wenye mtindio wa ubongo ya Queensland, iliyopo nchini Marekani, alisema: “wengi wa wagonjwa ambao wamekumbwa na matatizo hayo wamegundua ni wale waliowahi kutumia bangi kwa muda mrefu na hatimaye kujikuta wakipata tatizo la akili.”
Daktari huyo alisema kuwa ni nadra sana kukutana na wagonjwa wa akili vijana halafu wakawa hawajawahi kutumia bangi iwe mwaka mmoja au zaidi.
Alisema kuwa iwapo matumizi ya bangi yatakomeshwa tatizo la vijana kupata matatizo ya utahira yatapungua kwa kiasi kikubwa duniani.
Bangi ni nini, inatumiwaje?
Kwa hapa nchini na baadhi ya nchi, bangi imetambulika kama dawa za kulevya ambayo imekuwa na majina mengi kutokana na kutumiwa na kundi la vijana zaidi kuliko watu wazima.
Bangi imekuwa ikijulikana kwa majina mengi ikiwamo, Dawa, Ganja, Hashish, Kijiti, Marijuana, Kaya Blunt, na mengineyo ilimradi kutegemeana na sehemu inapotoka na watumiaji wengi wamekuwa wakiitumia kwa kuvuta kama sigara au wengine hutumia kwenye kiko kwa kuvuta.
Bangi ni bidhaa iliyochanganyika na kemikali hatari ambazo ni sumu ambayo huathiri afya kama vile ‘nicotine’ na nyingine hatari.
Wapo baadhi ya watumiaji wa bangi ambao wamekuwa wakiitumia kwa kuiweka katika maji wakiifanya kama majani chai na wengine huchanganya kwenye chakula.
Kwa vipi bangi inaathiri ubongo?
Wanasayansi wamebaini kuwa matatizo makubwa yanaanza kupatikana kutokana na bangi kuingia kwenye ubongo wa mtumiaji na kuathiri mfumo mzima wa akili.
Tatizo kubwa linalomkumba mvuta bangi ni kunyemelewa na magonjwa ya Ugonjwa wa Shinikizo la damu (BP), kupoteza kumbukumbu, Mawazo, anaridhika hata kama anamatatizo.
Pia mtumiaji wa kila siku anakuwa akikumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika ubongo wake.
Imebainika kuwa bangi inachangia kuongeza la mapigo ya moyo toka asilimia 20 hadi 100, muda mfupi tu wa saa tatu baada ya kuvuta.
Bangi huaribu mapafu kwani ina zaidi ya asilimia 50–70 ya kemikali aina ya carcinogenic hydrocarbons kuliko mvutaji wa tumbaju.
Mtumiaji wa bangi hupumua kwa tabu sana kuliko yule anayevuta tumbaku ingawa wote wanaharibu mapafu.
Mvutaji wa bangi anao uwezekano mkubwa wa kukaribisha ugonjwa wa kansa.
Imebainika kuwa watu wanaovuta bangi wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na matatizo mengi ya kiafya.
Madhara ya maisha ya kila siku
Watafiti wamegundua kuwa wavutaji wengi wa bangi wamekuwa hawana mahusiano mema na watu walionao karibu kwani wamekuwa chanzo cha matatizo kutokana na wao kuona kila wanachofanya wao ndiyo sahihi na cha wenzao si sahihi.
0 comments:
Post a Comment