
KARIBUNI katika safu hii ya nani ni nani ambayo hukupatia mambo mbalimbali kuhusu wanamieleka na leo katika safu hii utapata nafasi ya habari ambazo zimeenea zikimuhusisha mbabe Jeff kuwa na mipango ya kuhama Chama Cha Mieleka (WWE) na kumfuata nduguye katika Chama Cha mieleka (TNA).
Dalili za kuondoka kwa mbabe huyu zilianza kuonekana mara baada ya mwaka jana kaka yake Jeff Hardy kutangaza kuhama WWE pindi mkataba wake ulipomalizika WWE na kugoma kuongeza mkataba mwingine na muda mchache baadaye alitangaza kujiunga na TNA.
Hali kama hiyo imejitokeza kwa Matt Hardy ambaye alianza kukataa kuongeza mkataba WWE na badala yake akiomba kuruhusiwa apumzike.
Ombi lake hilo aliliomba tangu mwanzoni mwa mwezi uliopita liligonga mwamba kutokana na kudaiwa kuwa asubili kwanza amalize mkataba wake kwanza mwishoni mwa mwezi huu huku wakiendelea kumbembeleza.
Viongozi wa WWE walijikuta wakishindwa kumshawishi na kumuwezesha kubaki hapo na hatimaye Ijumaa iliyopita WWE ilitoa taarifa ya kumaliza mkataba na Matt Hardy mwishoni mwa mwezi huu.
Katika taarifa hiyo WWE iliyotoa ilimruhusu mbabe huyo kwenda katika chama chochote apendacho kwa matakwa yake na hawana neno naye kwa uamuzi wake.
Pamoja na kumuacha kwake lakini WWE imekiri kuwa imemuacha mbabe huyo huku ikiwa inamuhitaji kutokana na uwezo wake pindi awapo ulingoni.
Ili kuonyesha kuwa hatamani tena kupambana tena WWE, Hardy alifurahishwa na uamuzi huo na kusifia kwa kusema kuwa ni jambo jema kwa kuruhusiwa kwenda popote apendapo.
Mashabiki wa wawili hao wanasema kuwa uwezekano wa kuondoka kwake na kumfuata kaka yake ni mkubwa kutokana na historia yao ya kufuatana futana pindia anapokuwa ameondoka mmoja wao.
Kwa mara ya kwanza walikuwa kwenye Chama cha mieleka cha Organization of Modern Extreme Grappling Arts (OMEGA).
Lakini kwa mara ya kwanza Matt alisainiwa na WWE hivyo alianza kumshawishi mdogo wake, Jeff Hardy na hatimaye wote walijiunga WWE na waliunda kundi lililokwenda kwa jina la Team Xtreme.
Mbabe Matthew ‘Matt’ Moore Hardy aliyezaliwa Septemba 23, 1974 nchini Marekani amekuwa akifanya makubwa katika mieleka kwani ameshatwaa mataji kibao ya ubingwa ikiwamo ubingwa wa uzito wa juu wa dunia na Tag akiwa na kaka yake Jeff.
Hardy amefanikiwa kutwaa taji la uzito wa juu mara moja, bingwa wa ECW, WWE mara tano, Hardcore, Ulaya, Cruiser na Marekani.
Mchezo wa mieleka ameuanza akiwa Kihistoria Hardy, tangu alipokuwa kinda alikuwa akivutiwa na mchezo huu na alijikuta akianza kucheza mchezo huu kimataifa akiwa na miaka 15 pekee.
Wakiwa wanatumia jina la Hardy Boyz na kaka yake mwaka 1999 walitwaa ubingwa wao wa kwanza wa Tag wa WWF nah ii ni baada ya kuisambaratisha kambi ya Acolytes lakini baada ya mwezi mmoja walijikuta wakipoteza taji kwa kundi hilo.
Oktoba 17, 1999 wakiwa katika mapambano ya No Mercy, Hardy Boyz walishinda taji la Tag la WWF likiwa taji lao la kwanza la mashindano ya ngazi dhidi ya akina Edge na Christian.
Mwaka 2000, Hardy Boyz walipata Meneja mwingine aliyejulikana kama Lita ambaye aliwashauri wabadilishe jina lao na kujiita Team Xtreme.
Baada ya kutoa kipigo kwa akina Edge na Christian mwaka 2000 walitangaza vita ya kutaka kurudiana na timu hiyo ambako katika mechi ya marudiano walifanikiwa kutetea taji lao la WWF kwa mara nyingine.
Katika mapambano ya SummerSlam, kundi hilo likicheza katika mapambano ya meza, ngazi na viti maarufu kama (TLC), walifanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kuwachakaza akina Dudley Boyz, Edge na Christian.
Mwaka 2001, Hardy aliendeleza ubabe hapa akiwa mwenyewe alitwaa taji la ubingwa la WWF/WWE alipocheza dhidi ya Triple H.
Aliendelea kufanya mambo makubwa kwani mwaka huo alifanikiwa kutwaa ubingwa wa uzito wa juu wa Light dhidi ya Jerry Lynn.
Kwa kuonyesha kuwa hakuwa kijana wa mchezo mwaka huo akicheza dhidi ya Mike Awesome alifanikiwa kumchapa na kutwaa ubingwa wa Hardcore.
Juni 2009 Hardy alifanyiwa upasuaji wa mshipa wa mguu baada ya kuruka na kuumia kwenye mapambano ya SmackDown ambako alikuwa akimsaidia CM Punk aliyekuwa akipambana na Hart.
Mwaka huu katika mapambano ya ngazi ya Money in the Bank yaliyojulikana kama WrestleMania XXVI alitembeza kipigo kwa Drew McIntyre lakini hakushinda pambano hilo kutokana na Jack Swagger kuingilia na kushinda.
Kabla ya kujiunga na mieleka Hardy alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wa kikapu na soka katika kipindi chote cha masomo yake ya sekondari mpaka chuo kikuu na alikuja kuacha baada ya kunogewa na mieleka.
Mbabe Hardy bado hajaoa ila alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mbabe wa kike wa WWE, Diva Amy Dumas waliyekaa naye kwa muda wa miaka sita lakini walitengana kutokana na dada huyo kutembea na rafiki yake mkubwa ambaye naye ni mwanamieleka, Adam ‘Edge’ Copeland mwaka 2005 na sasa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mbabe mwingine wa kike, Diva Ashley Massaro.
0 comments:
Post a Comment