KARIBUNI wababe wenzangu mnaoisoma safu hii ya nani ni nani inayokuijia kila siku za Jumatatu kama ya leo na mbabe ambaye tutamzungumzia leo ni Edge.
Mbabe Edge ametoa kauli ya kusema kuwa anatarajia kuachia kustaafu kucheza mchezo ameushtua ulimwengu wa wapenzi wa Mieleka kwa kuwambia kuwa anatarajia kustaafu baada ya kuisha kwa miaka miwili.
Edge ambaye jina lake ni Adam Joseph Copeland, amefanikiwa kujikusanyia mashabiki kibao katika tasnia hiyo ya mieleka ametangaza nia hiyo akiwa na maana kwamba amebakisha mwaka mmoja na miezi sita.
Akielezea sababu ya kufikia uamuzi wa kufikiria kuachana na mchezo huo, Edge ambaye ni raia wa Canada alisema amejikuta katika wakati mgumu kila mara ambako amejikuta akipata majeraha.
Edge amesema kuwa pia ameanza muda mrefu kucheza mcheza huo tangu mwaka 1990 akiwa kijana mbichi mpaka sasa amekuwa mtu mzima anastahili kupumzika.
Edge alisema kuwa kustaafu kwake kutakuwa tofauti na wanamieleka wengine ambao wamekuwa wakitangaza kustaafu na baadaye wanatangaza kusaini katika vyama vingine vya mieleka.
“Hiyo miaka miwili niyotoa ya kustaafu itakapofika na kutangaza sitaonekana kabisa nikiwa ulingoni,” alisema.
Edge ambaye amekuwa hasimu mkubwa wa mbabe Undertaker ni mmoja kati ya wababe wa WWE ambao wanaheshimika ikiwa ni pamoja na kupambana mapambano makubwa ya Raw.
Kihistoria mbabe huyo alianza kujifunza mieleka mwaka 1988 akiwa chini ya wakufunzi ambao walikuwa wababe wa zamani, Daddy Siki na Bon Hutchinson.
Na ilipofikia mwaka 1990 alijiunga na chama cha mieleka cha North American Independent (NAP) ambako alionyesha uwezo wa hali ya juu ikiwa ni pamoja kutwaa mataji kadhaa ya ubingwa.
Ubora huo wa Edge ulimfanya aonekane na chama cha WWE ambako mwaka 1997 alitangaza rasmi kujiunga na chama hicho.
Baada ya kujiunga hapa ndipo jina lake likawa kubwa zaidi duniani hasa alipokuwa akipambana katika kundi akiwa na mbabe, Christian Cage.
Akiwa na kundi hilo walifanikiwa kutwaa mikanda kibao ya chama hicho ambacho wakati huo kilikuwa kikijulikana kama vile WWF.
Kundi lake na Cage walilipatia majina kibao ikiwamo na ‘High Impact’, ‘Suicide Blondes’, ‘Revolution X’, ‘Hard Impact’ na ‘Canadian Rockers’.
Kwa kuonyesha kwamba Edge hakuwa mpambanaji wa mchovu, Juni 1999 alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mabara wa WWF, taji ambalo lilikuwa la kwanza akiwa katika kampuni hiyo.
Agosti 1999, Edge na Cage waliweka rekodi ya kutwaa ubingwa saba za Tag za WWF ikiwa ni pamoja na ubingwa wa meza, ngazi na viti.
Wakati akiwa peke yake kwa ubabe wake, Edge alifanikiwa kushinda jumla ya mataji tisa, ikiwa ni pamoja na manne ya WWE na matano ya uzito wa juu, bingwa mara tano wa mabara ikiwa ni pamoja na kushikilia ubingwa wa Marekani wa WCW.
Kwa kuongezea Edge amewahi kutwaa mkanda wa Mfalme wa ulingoni wa mwaka 2001, bingwa wa kufuata pesa juu ya ngazi wa mwaka 2005 ikiwa ni pamoja na bingwa wa Royal Rumble wa mwaka 2010.
Kwa sasa Edge ni mmoja kati ya wapambanaji wanaounda kundi la La Familia ambalo nalo limejipatia umaarufu mkubwa.
Hivi karibuni Edge alikuwa haonekani ulingoni kutokana na kuuguza majeraha ya shingo yaliyokuw yakimsumbua aliyoyapata wakati akiwa ulingoni.
Ukichilia masuala ya mieleka mbabe huyu amekuwa akishiriki katika uigizaji wa filamu, ikiwa ni pamoja na kushiriki kutangaza vipindi maarufu vya televisheni ambavyo ni The Weakest Link, Mind of Mencia, Deal or No Deal na MADtv.

0 comments:
Post a Comment