
Mr Blue: mtoto kwangu ni kuongeza ukoo
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Heri Samiri ‘Mr Blue’ amesema kwamba kwake kujaliwa na mwenyezi Mungu kupata mtoto ni furaha kwani ni sawa na kujiongezea ukoo wake.
Blue ambaye aliwahi kutamba na wimbo wake wa ‘Mapozi’ amebainisha kwamba sababu ya kuona kupata mtoto ni kuongeza ukoo imechangiwa na kuwa na ndugu wachache.
Akizungumzia masuala ya muziki msanii huyo alisema baada ya kutesa vilivyo na wimbo unaokwenda kwa jina la ‘tilalila’ ameachia wimbo mwingine unaokwenda kwa jina la ‘Loose Contro’.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment