Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Thursday, July 5, 2012


Wasanii jitoleeni kuchangia wenye mahitaji


WIKI hii katika kona ya Vunja vunja tutakuwa na mada inayowahamasisha wasanii wa nchini kuwa na moyo wa kuchangia hasa kwa makundi ya watu wenye uhitaji.
Tabia ya kuchangia watu wenye mahitaji ni moja kati ya mambo yanayompendeza Mwenyezi Mungu hata kumwezesha mtoaji aweze kujipatia thawabu na kuongezewa zaidi ya kile alichokitoa.
Suala la kuchangia haliwahusu viongozi wa dini, taasisi za kijamii na mashirika ya kimataifa ya misaada pekee bali hata kwa waigizaji wanastahili kujitoa katika hilo kwa kushukuru kile wanachokuwa wanapata katika kazi zao.
Kwa hapa nyumbani wapo baadhi ya wasanii wanaokuwa wanajitolea ingawa wengi hawajajenga mazoea hayo kama ilivyo kwa wenzetu ambao mara kadhaa wamejikuta kutokana na hali yao ya kujitolea wamekuwa wakipewa tuzo.
Suala la kusaidia watoto yatima, watu wenye ulemavu, huduma za jamii ikiwamo utatuzi wa kuchangia ujenzi wa vituo vya polisi, shule na mengineo ya aina hiyo.
Kwa hapa Tanzania fani ya urembo wamekuwa wakionekana katika sekta hiyo ya kusaidia kuwa mbele pindi wanapokuwa wamemaliza mashindano yao hali ambayo imekuwa ikisaidia wengine kujikuta wakiendeleza utaratibu huo hata baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.
Kwa upanmde wa waigizaji ningependa kutoa rai kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli za kijamii kama alivyokuwa marehemu Kanumba na msanii Diamond the Platnum.
Kuchangioa si kwamba utapata sifa pekee bali pia inasaidia kujiongezea mashabiki zaidi katika tasnia hiyo ya filamu ndani na nje ya nchi na hata wengine wanaokuwa wakiitazama vibaya kazi hii kama uhuni wataiheshimu.
Mwisho.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text