
Biden aendelea kuwa mgombea mwenza wa Obama
NEW YORK, Marekani
IKULU ya Marekani imesema kwamba rais Barack Obama ataendelea kushirikiana na mgombea wake mwenza ambaye ni makamu wa rais, Joe Biden.
Msemaji wa Ikulu Jay Carney alisema aliwashangaa wale ambao wamekuwa na maoni ya kumtaka rais kumbalisha mgombea mwenza wake huo na kumchagua mwingine.
Wiki hii Biden alipowahutubia watu wenye rangi mbalimbali huko Virginia alisema kuwa, mageuzi ya maduka ya kubadilishia fedha yanayotakiwa na chama cha Republic yatawarudisha watu kwenye minyororo, maneno ambayo yametafsiriwa na chama cha Republic kuwa ni maneno ya kibaguzi, hivyo kinamtaka rais Obama asimchague Biden kuwa mgombea mwenza.
CNN
0 comments:
Post a Comment