Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, August 5, 2012

Romney amshambulia Obama huko Indiana

EVANSVILLE, Indiana
MGOMBEWA wa urais kupitia chama cha Republican, Mitt Romney amezishambulia sera za Rais Barack Obama kuwa zimeshindwa katika uokoaji wa uchumi wa Marekani.
Mgombea huyo alikiponda chama hicho katika kampeini zake zilizofanyika kwenye jimbo la Indiana, ambako katika hotuba yake alishambulia sera zilizotumiwa na Democratic kuwa zimeshindwa kuinua uchumi wa Marekani.
Akihutubia wananchi hao kwa kutumia ripoti ya Idara ya kazi ilieleza kwamba Marekani imefanikiwa kuongeza ajira 163,000 kwa mwezi julai ambako ni tathmini ya miezi mitano pekee. Katika taarifa hiyo inaonesha kuwa pamoja nja kuongeza kiasi hicho cha ajira lakini kumekuwa na watu wasiokuwa na ajira kwa asilimia 8.3 ukilinganisha na Juni ambako ilikuwa asilimia 8.2.
Romney alisema kuwa kwa kupitia rekodi hiyo inaonesha familia maskini zimepata wakati mgumu.
Romney aliieleza hadhira ya watu waliohudhuria hapo kwamba tatizo hilo limechangiwa na sera mbovu zilizosimamiwa na rais Obama.
Miaka minne iliyopita Obama aliwashangaza wamarekani kwa kushindea jimbo la Indiana na kuweka historia ya kuwa mgombea wa kwanza wa Democrat kutwaa jimbo hilo tangu kulikosa kwa zaidi ya miaka 40.
Wakati Mitt akiendelea na kampeini zake, kwa upande wa Obama alikuwa akisherehekea miaka 51 ya kuzaliwa kwake siku ya jumamosi.
Mwisho.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text