Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Saturday, August 31, 2013

ATMET: Tiba asili itajwe na katiba

BARAZA la Katiba la Chama cha Watabibu wa Tiba Asili Tanzania (ATMET-Tanzania), limependekeza neno Tiba Asili litajwe katika Katiba mpya.
Akizungumza kwenye mkutano wa majumuisho ya maoni ya Rasimu ya katiba yaliyotolewa na Baraza hilo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,  Naibu Katibu wa ATME, Athumani Shem alisema maoni hayo yatakabidhiwa kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Alisema pendekezo hilo ni miongoni mwa mapendekezo yaliyokusanywa kutoka mikoa 25 na wilaya 133 za Tanzania Bara wakitambua kwamba Tiba Asili ni taaluma kamili inayojitegemea kimuundo na kimaudhui ambayo ndiyo chanzo cha tiba zote duniani.
“Huduma ya Tiba Asili ni huduma ya Afya hivyo kuna umuhimu wa kutajwa kwenye katiba ya jamhuri ya muungano” alisema Shem na kuongeza kuwa baada ya majumuisho hayo wangeyawasilisha na kuyabidhi maoni hayo ya waganga na wakunga kwenye Tume ya mabadiliko ya Katiba hivi karibuni. 

Akizungumzia changamoto hizo Shem, alisema ATME inakabiliwa na ukosaji wa fursa kushiriki mikutano ya ndani na Kimataifa inayohusu huduma za Afya, Tiba Asili, Tiba Mbadala, mapendekezo na maombi yao  mbalimbali  kutopewa majibu kwa wakati

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text