Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Saturday, August 31, 2013

Marekani yapata pigo Syria

DAMASCUS, Syria
HATUA Uingereza kutangaza kujiondoa miongoni mwa nchi zitakazoshiriki katika kumsaidia Marekani kwenye vita ya kuiondoa serikali ya Rais Bashar Al Assad.
Hatua hiyo inayoonekana kuwa pigo kwa Marekani katika harakati zake za kuiondoa serikali ya Syria kijeshi iliingia dosari jana baada ya bunge la nchini Uingereza kukataa jeshi lao kuhusika na mzozo wa Syria.
Wazo hilo lilikataliwa na bunge la nchi hiyo baada ya kukataa kupitisha mswaada uliokuwa umepelekwa na Waziri  Mkuu David Cameroon ukiwashawishi wamuunge mkono waziri huyo kushiriki katika vita hivyo ili aweze kumsaidia mshirika wake mkubwa Rais Barack Obama wa Marekani.
Wakizungumzia kuhusu hatua hiyo wachambuzi wa siasa za Kimataifa wanasema kuwa uamuzi wa wabunge wa Uingereza kukataa jeshi lao kuhusika na mzozo wa Syria ni pigo kwa Marekani ambayo italazimika kwa sasa kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa serikali ya Ufaransa ,Ujerumani na mataifa mengine makubwa.
Sababu ya wabunge wa Uingereza kuupinga mswada huo zinaelezwa kuchangiwa na kuhofia matokeo ya baada ya uvamizi huo ambao utaendeleza mauaji ya wananchi wa Syria na kusababisha mzozo huo kusambaa katika mataifa jirani kama ilivyokuwa kwa nchi za Iraq na Libya.
Kauli kama hiyo pia imezungumzwa na waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel aliyesema kuwa baada ya uamuzi huo wa bunge la Uingereza kugoma kushiriki, Marekani itaendelea kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa mataifa mengine ili kuichukulia hatua serikali ya Syria kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia wake.
Marekani imeituhumu Syria kwa kutumia silaha za kemikali kwa kuwavamia raia wake wasiokuwa na hatia, na kuvunja sheria za kimataifa kuhusu silaha hizo, tuhuma ambazo serikali ya rais Bashar Al Assad imeendelea kuzikanusha.
Nchi ya Ufaransa imeonekana kuunga mkono matumizi ya jeshi nchini Syria baada ya Rais wan chi hiyo, Francois Hollande kunukuliwa akisema kuwa kinachoendelea nchini humo hakikubaliki huku akishauri kutumia nguvu ya jeshi.

Rais Bashar Al Assad amesema kuwa tishio la Marekani la kusema kwamba ikiwa uchunguzi utabaini silaha hizo zilitumiwa, italazimika kuingilia mzozo huo kijeshi ni jambo ambalo halikubaliki kamwe na yuko tayari kujilinda.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text