Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Wednesday, August 28, 2013

Sadick: Watanzania hatuaminiki kimataifa


MKUU wa mkoa wa Dar es Saalam, Said Meck Sadick amesema Watanzania hawaaminiki Kimataifa kutokana na hivi karibuni kukamatwa kwa baadhi yao wakituhumiwa kujihusisha na ufanyaji wa biashara za dawa za kulevya.
Hayo aliyasema jana, jijini Dar es Salaam alipokuwa akihutubia mkutano wa wadau wa habari ulioandaliwa na Chama wa wanahabari wa Dar es Salaam (DCPC), na kusema kuwa mwanzo wakati watanzania walipokuwa wakisafiri nje ya nchi walikuwa wakiaminika kuliko watu wa mataiafa mengine.
Alibainisha kuwa doa ambalo limechangia kutoaminika limetokana na kukamatwa kwa baadhi ya Watanzania wakijihusisha na biashara hiyo.
Aliongeza kwamba hapo mwanzo Watanzania hawakuwa wakikaguliwa kwa kiwango cha juu kama ilivyo sasa kutokana na kuaminiwa kwao ambako wakati mwingine haikuwalazimu kugongea viza zao hapa nchini bali waliruhusiwa hata kugonga nje ya nchi.
Akizungumzia hatua za kuchukua kumaliza tatizo hilo alisema kwamba vita hiyo haitaweza kufanikiwa iwapo itaachiwa ishughulikiwe na serikali peke yake bali kila mtanzania ashiriki kuwafichua wafanyaji.
“Tunachotakiwa ni kuwaomba wanahabari na Watanzania washirikiane na serikali kuwataja wale mapapa wanaowafahamu wakijishughulisha na biashara hiyo ili wafikishwe katika vyombo vya sheria na kuchukulia hatua pindi watakapopatikana na hatia,” alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Akizungumzia kuhusu umuhimu wa wanahabari nchini Mkuu huyo wa mkoa, anawaona kama nguzo muhimu kwa jamii kutokana na ukweli kwamba Wananchi wengi wanawaamini kama ilivyo viongozi wa kidini.
Alisema iwapo wanahabari watatumia kalamu zao vibaya kwa maslahi yao au ya mtu fulani wanaweza kujenga au kubomoa iwapo wataandika habari isiyokuwa ya kweli.
Katika suala la mifarakano ya kidini, Mkuu huyo wa Mkoa alikiri kuwepo na kuongeza kuwa imeshasababisha kutokea mapigano kwa baadhi ya maeneo baada ya kuwepo kwa hali ya kutoelewana baina yao.
Alitoa wito kwa wanahabari kuepuka kuandika habari za uchochezi ambazo zitaamsha hisia za makundi na kutugawa hasa kwa misingi ya kidini kwani hata machafuko yanapotokea hakuna anayefaidika zaidi ya kupata hasara..     


0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text