
MWANASIASA
mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwilu amewashangaa baadhi ya watu
wanaozungumzia urais wa Tanganyika kwenye mchakato wa katiba mpya huku wakishindwa
kutafakari kutengeneza katiba itayomaliza tatizo la elimu na umasikini
uliyokithiri nchini.
Mkongwe
huyo aliyasema hayo Agosti 28, 2013 wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano
wa majumuisho ya maoni ya rasimu ya katiba ya Baraza la Chama cha matabibu wa
Tiba Asili Tanzania (ATMET-Tanzania), Bagamoyo mkoani Pwani.
Kingunge
alisema tangu kusomwa kwa rasimu hiyo hajasikia baadhi ya wanasiasa
wakizungumzia umasikini unaowakabili Watanzania milioni 15 huku theluthi moja
ya wananchi wote wakiwa hawajui kusoma.
Alisema
mkoloni alipoondoka watu waliyokuwa hawajui
kusoma walikuwa asilimia 80, baadaye asilimia 90 wakawa wanajua kusoma
lakini leo viongozi walioko madarakani hali katika sekta ya elimu ni mbaya na
kufanya idadi ya watu wasiyojua kusoma inaongezeka kwa kasi.
Kingunge
alisema wanapozungumzia katiba ina maana kwamba wananchi wanataka Katiba bora
ili kuondoa upungufu lakini hadhani kama watafanikiwa kutokana na mpango wa
wakubwa kujadili kurudisha majina ya nchi ambayo yalishafutika tangu mwaka
1964.
“Rasimu
hii hazungumzii kuondoa matatizo yanayomkabili mwananchi masikini ambaye
anaishi kwa mlo wa dola moja kwa siku haya ni matatizo makubwa”alisema.
Akizungumzia
muungano Kingunge, alisema kuzungumzia serikali tatu ni sawa na kuanzisha
mivutano, ambapo anaamini Tanganyika wakati huo lazima itataka kuwa zaidi ya
serikali ya Muungano.
Aliongeza
kuwa muungano huo umefanikiwa kwa kujenga umoja na kujenga utaifa ambao ni
mfano kwa nchi za Afrika.
Kingunge
aliongeza kuwa bado kuna umuhimu wake wa kuendelea kutumia fursa ya mabalaza ya
katiba yakatumiwa kuamua Katiba mpya unayotafutwa uweje ambayo ni haki ya
Watanzania.
Kwa
upande wa Tuba asili aliwataka wataalami hao kuingeza kituhada katika kufanya
tafiti ambazo zitasaudia kwa ajili ya kuisaidia serikali katuka sekta ya afya.
Alisema
sio vyema wakabweteka wakisubiri hadi wapewe fedha na wazungu ndio wafanye
utafiti kwa ajili ya kugindua tiba mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment