Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Monday, September 30, 2013

Mahafali yatumika kupiga kampeini

MAHAFALI ya darasa la saba katika shule ya msingi Saranga yamejikuta yakigeuzwa sehemu ya Kampeni za kujinadi kwa Kamanda na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Chris Kileo anayetajwa kutaka kuwania jimbo la Ubungo kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi ujao.
Tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki, katika mahafali yaliyofanyika katika kata ya Saranga, Kimara Temboni jijini Dar es Salaam.
Mgeni huyo alifika akiwa amechelewa tofauti na ilivyotarajiwa na wenyeji wake ambao hata hivyo walikata tamaa ya kumsubiri na nafasi yake kumkabidhi diwani wa kata ya Saranga, Ephrahim Kinyafu (chadema) aliyekuwa mgeni mualikwa.
Wakiwa wanaendelea na shughuli zao katika mahafali hiyo mara ghafla mjumbe huyo wa NEC, alifika katika shule hiyo akiwa amevalia magwanda yanayovaliwa na makamanda wa chama hicho akiongozana na walinzi watano waliokuwa wamevalia sare za Green guard.
Hali hiyo ilizusha taharuki miongoni mwa wazazi na diwani Kinyafu aliyechukua uamuzi wa kuondoa katika eneo hilo kwa maelezo kwamba alikuwa akiwahi shughuli nyingine.
Baada ya kuondoka diwani huyo Tanzania Daima lilifanya mahojiano na diwani Kinyafu aliyeeleza sababu za kuondoka kuwa ni kushindwa kuvumilia kukaa pale huku akiona sheria zinavunjwa.
 “Siwezi kuendelea kukaa katika eneo ambalo naona, limevamiwa na watu wanaoeneza siasa mashuleni kinyume na taratibu za elimu,” alisema Kinyafu.

Kutokana na tukio hilo Tanzania Daima ilimtafuta Ofisa elimu wa Wilaya ya Kinondoni, Hussain Ramadhani kwa njia ya simu ili kupata utaratibu wa tukio hilo aligoma kulizungumzia na badala yake alisema tumtafute baadaye kwa sababu alikuwa kikaoni.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text