Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Tuesday, October 1, 2013

“serikali isitishe tathmini ya nyumba zate”

WAKAZI wa Mloganzila wilayani Kisarawe mkoani Pwani, wameitaka serikali kuahirisha tathmini ya mali zao hadi watakapoelezwa namna watakavyonufaika au athari zitajitokeza wakati utakapotumika upana wa mita 10 au 22.5, kutoka barabarani hadi kwenye mali zao.
Katibu wa wanakikiji hao, Clara Ibihya jana alieleza wasiwasi wao mbele ya Wakala wa Barabara (Tanroads), na Ofisa wa Tathimini wa wilaya, kuwa unatokana na mazingira yaliyopo katika uendeshwaji wake.
Alisema walichukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa tathmini inayofanyika sasa haijajumuisha mali na rasilimali zao kama vile mazao, majengo, ardhi na nyingine zilizoko ndani ya upana wa barabara.
Ibihya aliongeza kuwa mvutano huo unatokana wahusika wa mradi huo kutowashirikisha Wananchi kwa kupitia viongozi wao kitendo kinachowapa wasiwasi kuwa huenda kazi hiyo ikawa imevamiwa na walanguzi.
“Kutokana na malalamiko yaliyotolewa na wanakijiji wenzangu tumekubaliana na wajumbe kuwa hoja kuu ya mkutano huu iwe ni kukutana na wataalamu kutoka Tanroads kuhusu ufafanuzi wa mradi wa barabara,”alisema.
Ibihya alisema wanakiji hao walikubaliana kwa kauli moja kuwa fomu zote na picha zilizokuwa zimechukuliwa awali kwa ajili ya kufanyiwa tathmini zirudishwe kwa ajili ya makubaliano mengine.
 “Tunataka zoezi la tathimini lisitishwe mpaka hapo mamlaka husika itakapozungumza na Wananchi pia fomu zitakazotumika katika kujaza taarifa zao itumike kwa lugha ya Kiswahili na sio Kingereza,” alisema.
Alisema wakazi hao wanataka mchakato huo lazima ufuate taratibu kwa kuwashirikisha  viongozi wao wa Mkoa wa Pwani,  kwa sababu tangu awali  hawajashirikishwa hali inayowafanya wakose utetezi.
Mhandisi wa Tanroads Chacha Marwa, akiwa kwenye mkutano huo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu madai ya wakazi hao alisema kipindi hicho alikuwa hakujiandaa kujibu maswali bali alifika pale kwa ajili ya kufanya tathmini.
Naye mthamini wa Serikali kutoka manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, aliyetambulika kwa jina moja la Moleka, aliwaeleza wakazi hao kuwa alikuwa hajui lolote bali alikwenda kule kwa kazi moja ya kufanya tathmini.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text