Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, October 6, 2013

Aliyeongoza mashambulizi balozi za
Marekani Kenya, Tanzania akamatwa

NEW YORK, Marekani
MAJESHI ya Marekani yamefanikiwa kumtia kizuizini Mshirika wa Alqaeda Abu Al Anas Al Libi ambaye anahusishwa na kuongoza mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania.
Hayo yamethibitishwa na msemaji wa wizara ya ulinzi ya Pentagon ya nchini humo, George Little akisema Libi  ambaye jina lake kamili ni Nazih Abdul Hamed Al-Raghie kwa sasa anashikiliwa kisheria na jeshi la Marekani baada ya kufanyika kwa muendelezo wa operesheni za Marekani dhidi ya ugaidi na kwa sasa yuko kizuizini katika eneo moja nje ya Libya.
Kiongozi huyo wa kijeshi alikaririwa akizungumza katika kituo cha televisheni cha CNN kuwa operesheni ya kumkamata mtuhumiwa Libi inakibali na inatambulika na serikali ya Libya, ingawa vyombo vya usalama vya nchini Libya vimeeleza kutotambua tukio lolote la kutekwa au kukamatwa kwa mtu huyo.

Serikali ya Marekani ilitangaza donge nono la kitita cha dola za Marekani milioni 5 kwa yoyote ambaye angemfichua alipo gaidi Libi anayetajwa katika orodha ya magaidi wanaowindwa na nchi hiyo.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text