Makomando wa
Marekani wachemka kuishambulia Al Shabaab
MOGADISHU,
Somali
MAKOMANDO
wa Marekani wameingia nchini hapa na kufanya mashambulizi katika jengo
lililokuwa likiaminiwa kukaliwa na kiongozi wa kundi la Al Shabaab.
Mashambulizi
haya yamefanyika ikiwa ni wiki kadhaa baada ya kundi hilo kushambulia jengo la
kibiashara la nchini Kenya la Westgate.
Kundi
la makomando la nchini Marekani limeelezwa kufanya shambulizi katika Pwani ya
mji wa kusini mwa Somalia dhidi ya wapiganaji hao wa al Shabab.
Shambulizi
hilo lililenga kumuua kamanda wa ngazi za juu wa wanamgambo hao wa kundi la Al
Shabab aliyetajwa kwa jina la Abu Siyad anayeishi katika mji wa Baraawe.
Hayo pia yamethibitishwa na Waziri wa Mashauri ya nchi za
Nje wa Marekani, John Kerry aliyesema kuwa mashambulizi hayo yamefanywa na
wanajeshi wa kikosi maalumu cha Marekani nchini Libya na Somalia yanaonesha
dhamira ya serikali ya Marekani kuwasaka wale wanaohusika na ugaidi.
Naye
ofisa mmoja wa jeshi la Marekani amekiri kuwa vikosi hivyo vya Marekani havikufanikiwa
katika shambulizi hilo la kumuua kiongozi wa Al Shabaab.
Maofisa
wa Marekani wamesema kuwa shambulizi hilo lilipangwa wiki moja na nusu
iliyopita kutokana na kuchochewa na hujuma iliyofanywa na wanamgambo wa al
Shabab dhidi ya jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi mwezi uliopita.
Mashambulizi
hayo yamethibitishwa pia na msemaji wa kundi la al Shabab Abdulaziz Abu Musab aliyesema
kuwa makomando wa kigeni walivamia Pwani ya mji wa Baraawe kwa kutumia boti
mbili za kasi na kuanza kushambulia lakini hawakufanikiwa kufikia malengo yao.
Amesema
kuwa baada ya kushindwa kwa shambulio hilo iliwabidi Al shabaab wafanye
mashambulizi makali yaliyosababisha askari wa Marekani kukimbia baada ya
kuzidiwa.
Taarifa
nyingine zinasema kuwa katika shambulizi hilo nyumba moja ilibomolewa katika
mji Barawe unaodhibitiwa na wapiganaji wa Al-Shabaab kusini mwa Somalia.
Habari
zinaeleza kuwa sababu za kushambuliwa kwa nyumba hiyo zilichangiwa na kufikiri
kwamba alikuwamo kiongozi wa kundi la Al Shabaab kutokana na kulindwa na
wapiganaji wa kundi hilo.
Redio
ya Mogadishu ilielezea shambulizi hilo lililodumu kwa muda wasaa moja lilitokea
jana usiku kwa kutumia ndege za kigeni ikiwamo pamoja na askari wa maji.
Mji
wa Baraawe uko kilomita 250 kusini mwa mji wa Mogadishu, umekuwa ukidhibitiwa
na wapiganaji wa al-Shabaab kwa miaka kadhaa na umekuwa ukishuhudia
mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa vikosi vya kigeni.
0 comments:
Post a Comment