Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Tuesday, October 1, 2013

Walimu Ilala wataka maelezo madai yao

BAADHI ya walimu wa Shule za msingi katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, wameutaka uongozi wa wilaya kutoa maelelezo kuwa ni kwa nini wamekuwa wakicheleweshewa mshahara wao kila mwisho wa mwezi unapofika.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake na Tanzania Daima jijini, kwa masharti ya kutoandikwa jina lake gazetini, mwalimu huyo alisema wanaiomba Serikali Kuu kuiangalia hali hiyo ambayo inaonekana kuota mizizi.
Mwalimu huyo alisema vitendo hivyo vya kucheleweshewa mishara vimekuwa vikiendelea kwa mfano hadi sasa mshahara wa Septemba hawajaupata.
Alisema wanashangaa kuona kuwa wenzao wa Temeke na Kinondoni wamekuwa wakipokea mshahara kwa wakati kila mwezi, lakini kwa upande wao sio hivyo.
“Sisi utaratibu huu wa kucheleweshewa mishahara yetu unatukatisha tamaa kwa sababu kila wanapopitisha siku wajue wanatujengea mazingira magumu ya kutoamini katika jamii tunayoishi nayo huku mitaani kwani wengi wetu tunakopa tunauguliwa na wakati mwingine yote hayo yanategemea mshahara mwisho wa mwezi”alisema mwalimu huyo huku akiungwa mkono na wenzake.
Akizungumzia malalamiko hayo, Ofisa habari wa Manispaa hiyo, Tabu Shaibu, alisema baada ya kupata taarifa hizo, alifuatilia kwenye Idara ya Fedha ili kubaini tatizo liko wapi.
Alisema hata hivyo, wahusika walimueleza kuwa mshahara ulikuwa umeingizwa kwenye Accounti zao za Benki husika tangu Septemba 30.

“Kama kuna mwalimu ambaye hajaingiziwa mshara wake, basi ni suala la yeye kufuatilia ili tatizo tulijue na kulipatia ufumbuzi,”alisema Tabu. 

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text