William Jason Reso akiwa amezaliwa Novemba 30, 1973 akiwa na urefu wa mita 1.88 na uzani wa kilogramu 102.9.
Mwanamieleka huyu ambaye ni raia wa Canada ukiachilia mieleka pia ni muigizaji mzuri wa filamu.
Pia ni bingwa wa mkanda wa EWC mwaka huu ambaye kabla ya kurejea kwake WWE, amekuwa akicheza katika chama cha mieleka cha Total Nonstop Action Wrestling akitumia jina la ‘Christian Cage’.
Reso ameshawahi kutwaa ubingwa mara nne wa uzito wa juu wa WWE, bingwa mara tatu wa uzito wa juu wa NWA na bingwa mara mbili wa ECW.
Bingwa mara tatu wa uzito wa juu wa WWF, bingwa mara moja wa Ulaya, bingwa mara moja Hardcore na bingwa mara moja wa uzito wa juu wa WWF.
Pia amepata ubingwa wa Tag mara nane, kati ya hizo nane (saba akiwa na Edge, mara moja akiwa na Lance Storm.
Septemba 1994, Reso alijiunga na shule ya michezo ya mieleka ya Sullys Gym, iliyokuwa chini ya Ron utchinson.
Wakati Christian akianza mieleka kwa mara ya kwanza mwaka 1995 akicheza dhidi ya Keith Assoun "Zakk Wyld" na pambano hilo alitoka sare.
Mwaka 1997, alikuwa mmoja kati ya wanamieleka waliokuwa wakiunda kundi la THUG Life, lililokuwa na wasanii kama vile, Joe E. Legend, Zakk Wyld, Rhino Richards na Sexton Hardcastle.
Akiwa na Copeland kwenye kundi la "High Impact" walifanikiwa kutwaa taji la Tag la WWF.
Baada ya kucheza katika kiwango cha hali ya juu aliamua kutumia jina la Christian na mwaka 1998 alitwaa ubingwa wa uzito wa juu wa WWF katika pambano alilocheza na Taka Michinoku.
Baada ya kuonekana kuwa bora alitengeneza kundi akiwa na akina Gangrel na Edge lililopewa jina la The Brood.
Hakuweza kudumu na kundi hilo kwa muda mrefu kutokana na kutokea kwa hali ya kutoelewana baina yao na hatimaye alijiunga na mbabe, The Undertaker.
Walimaliza tofauti zao na Edge kwa mara nyingine Christian alirejea katika kundi lake la The Brood na pambanmo lao wakiwa kama kundi walicheza mwaka 2000 dhidi ya kundi la Hardy Boyz linaloundwa na ndugu wawili (Matt na Jeff Hardy).
Pambano hilo lilikuwa linajulikana kama ‘No Mercy’ lakini kundi la Hardy Boyz lilifanikiwa kushinda pambano hilo na Aprili 2, 2000 katika mapambano ya WrestleMania Edge na Christian walifanikiwa kulipiza kwa kulisambaratisha kundi la Hardy Boyz.
Pia mwaka huo walifanikiwa kutwaa ubingwa wa WWF wa tag baada ya kuliadabisha kundi la Dudley Boyz lililokuwa chini ya wababe (Bubba Ray na D-Von.
Katika pambano la Royal Rumble la mwaka 2001, Christian na Edge walijikuta wakikubali matokeo kwa kuachia taji lao la WWF kwa kundi la Dudley Boyz.
Baada ya kupoteza taji hilo walianza kazi ya kulitafuta na hatimaye walijikuta wakipokea kipigo kikali kutoka kwa Kane na Undertaker.
Mwaka 2001 Christian alitwaa ubingwa wa Ulaya wa WWF lakini alikaa nalo kwa muda wa mwaka mmoja na baadaye kuchukuliwa na Diamond Dallas Page.
Baada ya kupoteza kwa Page aliamua kuomba pambano la marudiano ambalo alijikuta akipoteza kwa mara nyingine kwa kukubali kupokea kichapo cha mbwa mwizi.
Oktoba 14, 2003 akiwa katika kundi moja na mbabe Jericho walifanikiwa kutwaa ubingwa wa WWF Tag.
Katika mwaka huo wa 2003 Christian alijikuta akichezea kipigo kutoka kwa Booker T aliyetwaa ubingwa wa Mabara.
Mwaka 2005 baada ya kumaliza mkataba wake WWF/E alitangaza kuhamia katika chama cha mieleka cha Total Nonstop Action Wrestling (TNA)
Wakati akiwa hapo TNA akitumia jina la Christian Cage aliingia kwa kushinda pambano lake alilocheza dhidi ya Bobby Roode na kutwaa ubigwa wa uzito wa juu wa NWA.
Februari 12, 2006 alitwaa ubingwa wa uzito wa juu wa dunia baada ya kumchapa Jarrett na mwaka uliofuata alipata ubingwa wa uzito wa juu wa NWA baada ya kumchapa Abyss.
Christian alifanikiwa pia kuitwaa ubingwa wa TNA baada ya kumchapa Joe na kuweka historia ya kushikilia kwa muda mrefu wa mwaka mmoja bila kunywang’anywa.
Christian alifanikiwa kutwaa ubingwa wa uzito wa juu wa TNA baada ya kumpiga A.J. Styles.
Novemba 13, 2008, Cage alicheza pambano na Booker T ambako alifanikiwa kutwaa ubingwa wa TNA na kuishia kupata majeraha na kutangaza kumaliza mkataba wake.
Januari mwaka 2009 alitangaza kurejea WWE kwa kusaini mkataba mpya.
Na mechi yake ya kwanza baada ya kurejea alimchapa Jack Swagger na kutwaa ubingwa wa ECW.
Katika maisha ya kawaida Christian ni rafiki mkubwa wa mbabe Adam ‘Edge’ Copeland ambaye walisoma naye masomo ya sekondari na pia kwa pamoja wanaishi katika eneo la Tampa, Florida.
Pia ni rafiki mkubwa wa mwanamieleka wa TNA, Terry ‘Rhino’ Gerin kwa miaka kibao.
Mke wa Christian ni Mjerumani anayejulikana kama, Denise Hartmann aliyefunga naye pingu, Mei 25, 2001.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
iws q alv e, free xxx. bnm a, vne eirlur! kyie y mhf mg.
Post a Comment