
KARIBUNI wapenzi wasomaji wa safu hii ya nani ni nani na leo tutamzungumzia kuhusu hatima ya mbabe ambaye amekuwa haonekani ulingoni kwa muda mrefu sasa, The Undertaker.
Kutooneka kwa mbabe huyo, kumechangia kuzuka kwa maneno mengi wengine wakidai amefariki lakini baadaye ilikuja kubainika kuwa alikuwa anauguza majeruhi aliyoyapa wakati akicheza pambano na Mysterio.
Hivi karibuni tena kumeibuka taarifa za kusikitisha kwa wapenzi na mashabiki wa mwanamieleka huyo anayechezea Chama cha Mieleka duniani (WWE).
Mbabe huyo alipata majeruhi ya bega wakati alipokuwa akifanya mazoezi ya kurejesha mwili wake katika hali ya kawaida nyumbani kwake.
Undertaker alijikuta akiangukia bega lake la kulia wakati akitembea na kusababisha kuumia na sasa amefanyiwa upasuaji.
Tatizo hilo limemfanya Meneja wa WWE, McMahon kulitolea taarifa na kusema kuwa ni vigumu kwa mbabe huyo kurejea hivi karibuni.
Alisema kuwa wababe hao wanatarajiwa kurejea ulingoni Aprili 3, mwaka huu katika pambano kubwa la 27 linalojulikana kama ‘WrestleMania 27’.
Mbabe huyo alikuwa ametarajiwa kupona na kurejea ulingoni mwishoni mwa mwezi huu lakini sasa uwezekano huo umeondoka kabisa na kutokana na kuumia kwa mara ya pili wakati alipokuwa akiuguza majeruhi.
Katika taarifa iliyotolewa na WWE kuhusu mbabe huyo ambaye anakwenda jina la Mark William Calaway aliyezaliwa Machi 24, 1965 imedai kuwa mbabe huyo amefanyiwa upasuaji mwishoni mwa wiki.
Hii inakuwa pigo kubwa kwa Undertaker ambaye hapo nyuma amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mguu alioumia katika pambano la dunia la Fatal 4-Way lililochezwa Aprili 6, 2010 akiwania mkanda wa PPV dhidi ya wababe Swagger, Punk, Big Show lakini alijikuta katika wakati mgumu na kuumia paada ya Rey Mysterio kuingilia na kumuumiza.
Katika mieleka mbabe huyu anahistoria ndefu kwenye mchezo huu ambao alijiunga mwaka 1984 akitumia jina la The Undertaker.
Mbabe huyo amefanikiwa kuwa na mvuto mkubwa tangu alipoingia kwenye tasnia ya mieleka kutokana na uwezo wake wa kushinda mapambano kibao ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa WCCW katika mwaka 1984 ambako alianza kucheza mieleka.
Ukiachilia ubingwa huo pia amefanikiwa kutwaa mataji ya WCW katika mwaka 1989 na 1990 na hata mwaka 2002 alipohama WCW na kujiunga na Shirikisho la mieleka duniani (WWF) alifanikiwa kutwaa ubingwa wa huo.
Unapomzungumzia The Undertaker unakuwa unamzungumzia mbabe aliyeanzisha mapambano ya majeneza ambayo yamepata umaarufu kwa mshindi kupatana kwa kumuweka mtu ndani ya jeneza.
Uwezo wake wa kupambana vema katika mchezo huo alijikuta akipewa jina la ‘the Deadman’.
Undertaker alifanya makubwa akiwa mwenyewe au akiwa kwenye kundi na wababe wenzake kama vile Kayfabe na mdogo wake, Kane likijulikana kama Brothers of Destruction.
The Undertaker amefanikiwa sana katika mieleka hali ambayo imemfanya aweke rekodi ya kuwa mbabe anayeongoza kwa kushinda mapambano mengi zaidi ya WrestleMania akiwa ameshashinda jumla ya mapambano 18.
Pia amefanikiwa kuweka historia ya kuwa mbabe pekee aliyefanikiwa kuweka rekodi ya kutopigwa kwa mara nyingi katika mapambano ya Wrestlemania.
Mbabe huyo amefanikiwa kutwaa jumla ya mataji saba ya ubingwa, nane yakiwa ya WWE na matatu yakiwa ya uzito wa juu wa dunia (WHC).
Ukiachilia mataji hayo pia amefanikiwa kushikilia taji moja la WWF Hardcore ikiwa ni pamoja na mataji saba akiwa katika kundi (Tag): Mara sita ya WWF na moja la WCW.
Hakuishia hapo Undertaker kwani mwaka 2007 alifanikiwa kutwaa mkanda wa Royal Rumble na kuwa mbabe wa kwanza kushinda pambano hilo katika pambano lililojumuisha wababe 10.
Wengi wamekuwa wakijiuliza kama kweli mbabe huyo huchanganya na mazingaombwe.
Mwaka 1997 walianzisha kundi na mdogo wake lililojulikana kama Brothers of Destruction na wakati huu aligunduliwa kwa mara ya kwanza alimchapa, Paul Bearer ambaye baada ya kumalizika kwa pambano alisikika akimlalamikia kumpiga kimazingaombwe.
Mara zote alikuwa akibisha kutumia uchawi ilikuwa siri yake na mwaka 1999 siri hiyo ilivuja baaad ya Undertaker kuibuka na kutangaza kuwa na Wizara ya nguvu za giza, akidai kuwa wanachama wake watakuwa wakitumia nguvu za hali ya juu kuliko wengine.
Katika majaribio ya nguvu zake alionyesha maajabu kwa kumchapa mbabe ambaye alikuwa mgumu kwa wakati huo, Austin na kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu wa WWF.
Ubabe wa The Undertaker ulikuwa si wa kawaida kwani alifanikiwa kufanya vema hata anapokuwa kwenye kundi lake jipya la UnHoly akiwa na kane na The Big Show walifanikiwa kuitwaa ubingwa mara mbili wa WWF katika mwaka 1999.
The Undertaker aliendeeleza ubabe wake kwani mwaka 2009 alitwaa ubingwa wa uzani wa juu (WHC) baada ya kumfundisha adabu kijana CM Punk.
Kimaisha Undertaker amefanikiwa kucheza jumla ya mapambano 800 ya Raw na mkewe wa kwanza alikuwa Jodi Lynn aliyefunga naye ndoa mwaka 1989 na kuzaa naye mtoto mmoja na mwaka 1999 alifunga ndoa Sara na kuzaa naye mabinti wawili.
Lakini waliachana mwaka 2007 baada ya kugundua alikuwa na mahusiano na mwanamieleka wa kike, Michelle McCool ambaye alikuja kumuoa baadaye Juni 26, 2010 na ndiye akawa mkewe mpaka sasa.
Tumuombee mbabe The Undertaker arejee katika hali yake ya kawaida
0 comments:
Post a Comment