
NEIL ALDEN ARMSTRONG
Mwanadamu wa kwanza kutua mwezini afariki dunia
*Obama amlilia na kuongoza rambirambi yake
NEW YORK, Marekani
VILIO, majonzi na simanzi imetawala nchini Marekani baada ya kutangazwa kwa kifo cha mwana anga maarufu duniani ambaye ameweka historia ya kuwa mwanaanga wa kwanza duniani kujivinjari mwezini mwaka 1969.
Taarifa za msiba huu zimetangazwa moja kwa moja na Rais wa Marekani, Barack Obama ambaye aliongoza shughuli za utoaji wa rambirambi wa msiba huo uliotokea juzi.
Mwanaanga huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 82 kutokana na matatizo aliyopata baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye moyo wake.
Katika salamu zake za rambirambi, Rais Obama amemuelezea Neil Armstrong kwamba ni mmoja kati ya mashujaa wakubwa wa Marekani, siyo katika wakati wake, bali katika historia ya nchi hiyo.
Naye mwana anga mwenzake ambaye walikwenda naye katika safari hiyo Buzz Aldrin, amemwagia sifa kwa kusema Armstrong alikuwa rubani na kamanda mahiri.
Katika salamu zilizotolewa na familia ya Neil Armstrong imeitaka nchi ya Marekani kuonesha heshima zao kwa kufuata mfano wake wa kujitolea kutumika, kufanikiwa pasipo kuishi katika hali ya majivuno.
Taarifa ya familia iliwakumbusha mashabiki wa mwanaanga huyo namna ya kumkumbuka kwa kusema "ukitembea nje usiku ukaona mwezi unatoa mwanaga, mfikirie Neil na umkonyeze."
Kihistoria
Neil Armstrong ambaye ni amezaliwa Agosti 5, 1930 na kufariki Agosti 25, 2012 kabla ya kuwa mwanaanga alikuwa mwanajeshi wa kikosi cha maji cha Marekani ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo ya urubani.
Armstrong amezaliwa na mama yake ambaye alikuwa mkulima wa jimbo la Ohio akiwa na asili ya Scotland na Mjerumani huku baba yake Stephen akiwa mkaguzi wa mahesabu wa jimbo la Ohio.katika familia yake walikuwa watatu ambako alikuwa na wadogo zake wawili ambao ni June na Dean.
Kutokana na shughuli za baba yake iliwabidi wawe watu wa kuhama ambako kwa miaka 15 pekee ya kuzaliwa walikuwa wamehama zaidi ya sehemu 20 tofauti.
Urubani kwa mwanaanga huyo haikuwa kazi ngumu kwa sababu alianza kupata mazoezi ya kuendesha tangu akiwa na umri wa miaka sita ambako alifundishwa na baba yake huko Ohio, alipofikisha umri wa miaka 15 tayari alikuwa ameshapata cheti cha urubani kabla ya kupata leseni ya kuendesha.
Baada ya kuona kazi hiyo ipo damuni aliamua kuisomea ambako mwaka 1947 alijiunga na chuo Kikuu cha Purdue kwa ajili ya masomo ya uinjinia wa anga na baaday kwenda chuo Kikuu cha Cambridge, Massachusetts kwa ajili ya masomo zaidi na baada kumaliza alipata nafasi ya kufanya kazi katika jeshi la maji la Marekani na mwaka 1952 alishiriki katika vita ya Korea.
Mwaka 1955 alifanikiwa kuajiriwa na Taasisi inayojishughulisha na mambo (ya Utafiti wa Anga nchini Marekani (NASA) akiwa rubani wa majaribio kwa aina mpya za ndege akiwa amemaliza Shahada ya Uzamili ya sayansi ya anga.
Januari 28, 1956 alifunga ndoa na mwanadada Elizabeth Shearon ambaye walifanikiwa kupata watoto watatu ambao ni Eric, Karen na Mark. Mkewe huyo alifariki Januari 28, 1962 kwa maradhi ya ‘homa ya mapafu’.
Akiwa amemaliza Shahada ya Uzamili ya sayansi ya anga katika chuo cha Southern California alijiunga na Taasisi ya Nasa akiwa katika kundi la wanaanga ambako safari yake ya kwanza ilikuwa Machi 16, 1966 akiwa mwanaanga kiongozi wa Gemini 8.
Kilele cha safari hii ilikuwa kukutana kwa Gemini 8 na satelaiti nyingine na kuunganisha vyombo vyote viwili kwa muda wa masaa kadhaa.
Safari ya kwenda mwezini
Baadaye aliteuliwa kuwa makamu wa kikundi cha wanaanga waliokwenda mwezini kwa kutumia chombo kilichoitwa Apollo 11.
Julai 20, 1969 Neil Armstrong pamoja na Edwin Aldrin ambaye alikuwa akimuona Armstrong kama shujaa wake walikwenda mwezini wakiwa wanadamu wa kwanza kufika huko na wa kwanza kutua mwezini alikuwa shujaa Neil Armstrong ndipo mwenzake huyo alifuatia.
Baada ya kufika huko walifanikiwa kutoka katika chombo huko angani na kuanza kutembea mwezini kwa mara ya kwanza.
Akiwa katika hali hii, Armstrong alidiriki kutamka maneno yafuatayo, "Hii ni hatua ndogo kwa mtu lakini hatua kubwa kwa ubinadamu."
Katika safari hiyo ilikuwa ikirushwa na kituo cha BBC na vituo vingine kiasi cha kufanikiwa kushuhudiwa na watu milioni 450 ambao walikuwa wengi kutokana na ukwewli kwamba idadi ya watu wa dunia kwa wakati huo ilikuwa bilioni 3.631
Baada ya kurudi salama, Armstrong alitangaza kuacha kazi NASA na badala yake akawa profesa wa uwanaanga kwenye chuo kikuu cha Cincinnati katika mwaka 1971 hadi alipostaafu na kujishugulisha na biashara zake.
Maisha yake
Mwaka 1992 alimchumbia Carol Held Knight na Juni 12, 1994 alifunga naye ndoa katika eneo la Indian Hill, Ohio. Mwaka 2010 alipewa heshima ya kuwa mwanaanga shujaa kuliko mwingine yeyote aliyewahi kutokea.
Baada ya muda mrefu kupita tangu atoke mwezini mwanaanga huyo aliripotiwa kubadili dini na kuwa muislam nah ii ilichangiwa na wakati alipokuwa juu alirekodi sauti aliyoisikia huko juu ambayo hakujua ilikuwa ikimaanisha nini.
Lakini alikuja kuijua baada ya safari yake ya kwenda Misri na aliisikia ikitoka msikitini na alipomuuliza rafiki yake wa Misri alimwambia ile ni adhana ambayo hutumiwa na waislam kuitana kwenda kusali.
Baada ya kupewa maelekezo hayo akaamua kuwa muislam na kutoa ushuhuda kuwa sauti hiyo ndiyo aliirekodi huko juu.
0 comments:
Post a Comment