Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Wednesday, September 5, 2012


Janga la kuvuja mionzi ya nyuklia Japan la kutengeneza
TOKYO, Japan
UNAPOZUNGUMZIA majanga ambayo yamewahi kutokea Japan na kuingizwa katika historia yaliyosababishwa na madhara ya Teknolojia yake ya urutubishaji wa vinu vyake vya nyuklia huwezi kuliacha lile la kulipuka kwa vinu vya Fukushima, ikiwa ni matokeo ya tetemeko la ardhi na Tsunami yaliyotokea Machi 11, 2011 na kuweka historia ya kuwa jangwa kubwa zaidi kwa nchi hiyo tangu kutokea kama la aina hiyo mwaka 1986 la Chernobyl.
Ulipukaji wa kinu hicho cha Nyuklia wa Fukushima Daiichi, uliofanyika ulisababisha watu 11 kuathirika na mionzi ya nyuklia papo hapo mara baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Baada ya tukio hilo ililipotiwa kuwepo kwa watu zaidi ya 590,000 kuyahama makazi yao kwa kuhofia usalama wa maisha yao.
Huku mzozo wa nyuklia ukiendelea kukumba nchi ya Japan, shirika la Afya duniani ilitoa taarifa iliyosema kuwa mionzi ya nyuklia ilionekana kuwa katika chakula kwa kiasi kikubwa.
Hali hiyo ilisababisha serikali ya Japan kuwataka wakulima na wazalishaji wengine katika maeneo karibu na vinu vya Fukushima kutouza mazao yao katika maeneo mengine.
Wanyama nao wa nchini hapo waliathiriwa kutokana na kula mboga na majani hayo yaliyokuwa yameathiriwa.
Atahari hizo hazikuishia hapo bali iliendelea hadi kufikia kampuni ya umeme ya Tokyo kutangaza kwamba wamegundua maji yenye mionzi ya nyuklia ilikuwa ikimiminika baharini baada ya juhudi za kuziba ufa uliogunduliwa kwenye ukuta wa kisima karibu na kinu kimoja cha nyuklia cha Fukushima kushindikana kuzibika.
Wakati hayo yakiendelea vinu vingine vikaendelea kuharibika ambavyo ni namba mbili ambacho kilikuwa tatu kulipuka katika kipindi cha siku nne kwenye mtambo huo wa Fukushima Daiichi.
Ulipukaji haukuishia hapo bali uliendelea na moto nao ulizuka ghafla katika kinu nambari 4 ambayo nayo ilivujisha mionzi zaidi.
Pamoja na kutokea kwa milipuko hiyo yote ambayo ilielezwa hapo mwanzo kwamba ilichangiwa na tatizo la majanga hayo ya Tsunami lakini sasa imebainika kwambatukio hilo lilikuwa janga la kutengenezwa na binadamu na halikuchangiwa na tetemeko la chini ya bahari Tsunami kama ilivyokuwa inaelezwa.
Hayo yamebainishwa na jopo lililoundwa na Bunge nchini Japan kwenye ripoti yake baada ya kufanya uchunguzi wa kina kubaini madai yaliyokuwepo awali ya kwamba janga hilo la kuvuja kwa mafuta limechangiwa na Tsunami.
Matokeo ya Uchunguzi huo yanaonesha uwepo wa kutokuelewana baina ya Serikali na Shirika la TEPCO ambalo linasimamia masuala ya nyuklia na kitu ambacho kilichangia pakubwa kila upande kushindwa kutekeleza majukumu yake.
Uchunguzi huo umesema kile ambacho kimefanyika ni usaliti kwa Taifa na hivyo kuchangia kuzuka kwa janga hilo la kuvuja kwa nyuklia na hivyo wamehitimisha kwa kusema ni janga ambalo limetengenezwa na binadamu.
Jopo hilo bila ya kung'ata maneno limesema kuwa wanaamini chanzo cha tatizo hilo ni Shirika la TEPCO kushindwa kupata masaada unaofaa kutoka kwenye mfumo wa Utawala na hivyo kuibuka kwa tatizo hilo.
Uchunguzi huu unaanza kuondoa wingu zito ambalo limekuwa likitanda tangu kutokea kwa janga la kuvuja kwa mionzi ya nyuklia nchini Japan kitu ambacho kilichangia hata baadhi ya vyakula vyake kupigwa marufuku kutumika.
Kabla ya kutolewa ripoti ya uchunguzi huu Shirila hilo la Umeme na nyuklia la TEPCO lilijisafisha na kusema kuvuja kwa mionzi ya nyuklia kulichangia kwa kiasi kikubwa na ukubwa wa tetemeko la chini ya bahari lililopiga nchi hiyo mwaka jana.
Ripoti hii ya Bunge inaweza ikatumika vizuri katika kuhakikisha wanachukua hatua dhidi ya wale wote ambao wamehusika kwenye uzembe ambao umechangia kwa kiasi kikubwa kuvuja kwa mionzi hiyo ya nyuklia kutoka kinu cha Fukushima.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text