Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Saturday, September 22, 2012

Kwa filamu hii, Lulu aliyajua mateso yake kabla KESI ya Lulu ni moja ya habari ambazo zimefanikiwa kutikisa hivi sasa katika vyombo vya habari kutokana na msanii huyo kuhusishwa na kosa la mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba. Kesi hiyo ambayo kwa mara ya kwanza ilifanikiwa kuteka hisia za wapenda burudani kutokana na tukio hilo kuwahusisisha wasanii hao wakubwa wa tasnia ya filamu. Kama kuna mtu ambaye amefanikiwa kuitazama filamu inayokwenda kwa jina la 'Women of Principle' ambayo ukiachana na tatizo la lugha iliyotumiwa ambako naamini walidhamiria kuiita ' Disciplined Women’ filamu hii imezungumzia maisha halisi ya Lulu kwa asilimia 80. Filamu hiyo imemzungumzia Lulu kama msichana aliyekuwa akiishi na mama yake mzazi ambaye alkikuwa akimtumia katika kujipatia kipato ingawa sitaki kusema kuwa msichana huyo alikuwa akitumiwa na mama yake mzazi kwa ajili ya kujipatia kipato cha familia. Ukiachilia hiyo pia kuna kipande ambacho kinamuonesha lulu mahakamani ambako katika hali halisi amepanda lakini katika filamu amepanda akiwa na mama yake ambaye kwa pamoja walimshtaki Ray aliyekuwa akilalamikiwa kwa kosa la kufanya mapenzi na binti mdogo ambaye alidaiwa kutofikisha umri wa miaka 18 na alimuachisha shule. Katika hali halisi baada ya Lulu kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Kanumba lakini mawakili wake walikuwa wakipinga mwigizaji huyo kupandishwa katika mahakama ya watu wazima na badala yake ashtakiwe katika mahakama ya watoto kwa sababu alikuwa hajafikisha umri wa miaka 18. Kama ilivyokuwa katika filamu hiyo wakati Ray anakutana naye na kuanzisha uhusiano wao wa kimapenzi, msichana huyo alimdanganya kwa kusema kuwa shule aliacha muda mrefu na umri wake ulitosha kabiusa kuwa na Ray lakini baada ya kutokea matatizo alimkana na kusema umri wake ulikuwa chini ya miaka 18. Pamoja na kuwa filamu nzuri lakini ilimalizwa kizembe huku ikiacha maswali lukuki ikiwamo; Nini hatma ya maisha ya Lulu na familia yake ambayo ilikuwa ikimtegemea Ray kwa matumizi yao ya kila siku? Swali jingine ni kwamba, Baada ya familia kugundua aliyekuwa mke wa Ray alitengeneza kesi na kumfunga hali iliyosababisha kutengwa na wazazi wake nini kiliendelea pale je, aliomba msamaha? Au aliendelea na maisha yapi baada ya kupimwa na kugundua alikuwa tayari na ujauzito wa Ray? jambo jingine kwa kesi ambazo zimekuwa zikisimamiwa na wanasheria zinakuwa makini kwa asilimia kubwa lakini katika filamu hiyo ilionesha namna ambavyo mawakili wa Ray hawakuonesha umakini katika kesi hiyo. Kwa nini nasema hawakuonesha umakini? Kwanza kwa namna ninavyowaelewa mawakili hakuna mjinga ambaye angeruhusu kesi kuendelea kusimamia kesi hiyo wakati anajua fika hakimu wake alikuwa ni mtalaka wa mshtakiwa waliyetengana naye kwa ubaya huku mkewe akiwa ndiyo kwanza amerudisha mapenzi kwa mumewe ambaye mwanzo alikuwa hana mapenzi naye kutokana na kubanwa na kazi za mahakamani. Sehemu nyingine ambayo haikuangaliwa kwa makini ni namna ambavyo mkewe alikuwa kazini alishindwa kuvaa mavazi kama yale ambayo hakimu amekuwa akiyavaa. Kwa maoni au ushauri simu namba 0717 368 668.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text