Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Friday, September 7, 2012


Mwaka huu wa AY
*Ateuliwa tena kuwania tuzo tatu channel O


MWAKA huu umeonekana kuwa wa mafanikio kwa msanii Ambwene Yesayah (AY) ambako baada ya kupata zali la kutangazwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kuwa balozi wake mpya kwa mwaka 2012-2013.
Katika dili hilo AY amepata nafasi hiyo ambayo kwa mwaka jana ilikuwa ikishikiliwa na Ali Kiba ambaye aliungana na wasanii wengine wa kimataifa akiwamo R. Kelly katika kundi lililopewa jina la One8.
AY kwa sasa ni msanii wa Kimataifa aliyefanikiwa kuipaisha bendera ya Tanzania katika nchi mbalimbali kwa kufanya shoo ambazo si za kawaida kama ilivyo kwa wasanii wengine wanapokwenda nje ila yeye amekuwa akifanya matamasha ya kimataifa katika nchi mbalimbali kama Marekani, Uingereza, Hispania, Dubai, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Malaysia, India, Russia, Afrika Kusini, Kenya na Uganda.
Kutokana na kufahamika kimataifa AY ameweza kufanyakazi na wasanii wengine wakubwa wa kimataifa kama vile Chameleon, Ngoni wa Uganda, Amani, Nameless, Jua Cali (Kenya), P. Square, J. Martins (Nigeria), Ms. Trinity, Sean Kingston, Lil Romeo wa Marekani.
Uwezo wa AY katika fani hii ya muziki ulijidhihirisha kwa kutajwa kuwa msanii wa kwanza aliyeweka rekodi ambayo haijavunjwa ya kuwa msanii wa kwanza kiume Tanzania, kutunukiwa tuzo ya KORA mwaka 2005.
Ukiachilia tuzo hiyo aliyoipata ya KORA pia amewahi kupata tuzo ya kimataifa ya MTV MAMA aliyopewa mwaka 2009 na mwaka 2010 aliyopewa na France.
Kwa kuonesha kwamba AY hafanani kiuwezo na msanii mwingine wa hapa nchini kwa mwaka huu amechaguliwa tena kuwania tuzo za Channel O katika vipengele vitatu vya video bora ya Afrika Mashariki ya mwaka, video bora ya mwaka na mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka.
Tuzo hizo zimetangazwa kufanyika Novemba 19, 2012 na Nigeria ndiyo imeongoza kwa kuingiza wasanii wengi wanaofikia 13 ambao ni 2face, D’banj, Psquare, Wizkid, Wande Coal, Davido, Mo’Cheddah, Brymo, Orezi, Tiwa Savage, rapa Naeto C, Ice Prince na Dbanj.

Chini ni orodha ya wasanii wanaowania tuzo hizo
Video bora ya mwaka ya eneo la kusini
Cashtime Fam – Shut it down (Stundee)
HHP – Bosso
Shota ft Shana
Zeus – Dancing Shoes
Paul G ft Maezee – The Feeling
Shugasmakx ft Moneoa – Take it Easy

Video bora ya hip hop ya mwaka
Khuli Chana feat Notshi – Tswa Daar
L-Tido – Smash
Ice Prince – Superstar
M.Anifest – Makaa Maka
K’NAAN feat Nas – Nothing to lose

Video bora ya mwaka ya Afrika Magharibi
D-Black ft Mo’Cheddah – Falling
Wizkid – Pakurumo
Sarkodie feat Obrafour – Saa Okodie No
Naeto C – I gentle
Wande Coal – Private trips
Video bora ya mwaka ya R&B
Lloyd Cele – Hero
Lizha James ft Perola – Leva Boy
Flavour feat Tiwa Savage – Oyi
2Face – Be there
Habida feat Cannibal – My Reason

Video bora ya mwaka ya Afrika Mashariki
Keko feat Madtraxx – Make You Dance
Camp Mulla – Party Don’t stop
AY feat Sauti Soul – I Don’t Want to Be Alone
K’Naan and Nas – Nothing to lose
Navio – One & Only

Video bora ya msanii aliyodansi ya mwaka
DJ Zinhle feat Busiswa – My name is
DJ Cleo – Facebook
OS3 feat Tchoboly – Mokongo
Davido – Dami duro
Bucie – Get over it
Cpwaa – Hnmm

Video bora ya msanii chipukizi
Toya Delazy – Pump it on
Davido – Dami duro
E.L. – Turn the lights down
Camp Mulla ft – Party don’t stop
Donald – I deserve

Wimbo bora wa midundo ya kiafrika
Jozi – Ugologo
DJ Sbu ft Zahara -
Gal Level feat Toniks – Money
Brymo – Ara
Maurice Kirya – I don’t Want to Fight

Video bora ya Reggae ya mwaka
HHP feat Lutan Fyah, Omar Retnu – Baheitane (remix)
Buffalo Souljah ft Cabo Snoop – Styra Inonyengesa
Ice Prince – Juju
Orezi – Booty Bounce
Wyre – Dancehall party

Video bora ya Kwaito ya mwaka
Kabelo ft Professor: Amapantsula’Ajabulile
Spikiri ft Various Artists – Ngeke Balunge
Big Nuz – Serious
Ees feat Mandoza – Ayoba
The Dogg ft Brickz – Tromentos

Video bora ya mwaka
Dj Zinhle ft Busiswa – My name is
Khuli Chana ft Notshi – Tswa daar
Toya Delazy – Pump it on
Lizha James feat Perola – Leva boy
Big Nelo: Sente o beat
D’banj – Oliver twist
Brymo – Ara
Sarkodie feat Obrafour – Saa Okodie No
Camp Mulla – Fresh all day
AY feat Romeo, Lamyia – Speak with your body

Video ya mwimbaji bora wa kike
Zahara – Loliwe
Lizha James feat Perola – Leva body
Tiwa Savage – Love me love me love me
Mo’Cheddah feat Phenom – See me
Keko feat Madtraxx – Make you dance

Video ya mwimbaji bora wa kiume
Khuli Chana ft Notshi – Tswa Daar
PRO – Makasana
Big Nelo – Sent
D’banj – Oliver twist
Ay feat Romeo and Lamyia – Speak with your body

Video ya kundi bora la mwaka
Mi Casa – Heavenly sent
Liquideep – Still
Camp Mulla – Fresh all day
Buffalosouljah ft Cabo Snoop – Styra Inonyengesa
Psquare feat Akon, May D – Chop my money
Credits: thenetng

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text