NAIROBI,
Kenya
TAKRIBANI
watu 41 wameelezwa kuuawa baada ya basi moja la abiria lililokuwa likitoka
Nairobi kuelekea Homabay Magharibi mwa Kenya kuanguka na kubingirikia mara
kadhaa kabla ya kupata ajali eneo la Narok.
Taarifa
kutoka kwa mkuu wa jeshi la polisi wilayani Narok Patterson Maelo imesema kuwa miongoni
mwa waliokufa ni pamoja na watoto wanne huku dereva wa basi hilo alishindwa
kulithibiti katika eneo la kona na hivyo basi hilo kupoteza mwelekeo na
kuanguka.
Maofisa
wa shirika la msalaba mwekundi ambao tayari wamefika katika eneo la tukio hilo
wamesema kuwa watu wengine 33 waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali ya wilaya ya
Narok kwa matibabu.
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni wa viongozi waliotuma risala zao za rambi
rambi kwa jamaa na marafiki wa abiria waliouawa.
Katika
ripoti iliyochapishwa kwenye mtandao wake wa twitter, rais Kenyatta ametoa amri
kwa idara ya polisi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa magari ya umma
wanaokiuka sheria za barabarani.
BBC
0 comments:
Post a Comment