LONDON,
Uingereza
KIONGOZI
wa chama cha Upinzani cha Labour, nchini hapa, Ed Miliband, amesema bunge la
nchi hiyo halipaswi kuamua ikiwa itaidhinisha mzozo wa Syria kutatuliwa
Kijeshi.
Milliband
ameyasema hayo muda mfupi kabla ya bunge la Uingereza kupiga kura ikiwa nchi
hiyo kama itaishambulia Syria, kutokana na madai ya kutumia silaha za kemikali
mjini Damascus.
Waandishi
wa habari wanasema kuwa serikali ya Uingereza inahofia huenda ikapoteza kura
hiyo na hivyo kukosa idhini ya kuingilia mzozo huo wa Syria.
Milliband
amesema wamejifunza mengi kutokana na maamuzi yaliyochukuliwa miaka ya zamani
kama ule wa kuivamia Iraq.
Amesema
jamii ya kimataifa inapaswa kulipa jopo maalum na wachunguzi wa Umoja wa
Mataifa nafasi ya kufanya kazi yao.
Serikali
ya Uingereza imesema ina habari za kijasusi kuhusu Syria na itachapisha ripoti
hiyo na ushauri wa kisheria kabla ya mjadala huo kuanza bungeni.
BBC
0 comments:
Post a Comment