KINSHASA,
DRC
UMOJA wa
Mataifa (UN), umesema kuwa mwanajeshi wake mmoja wa kutunza amani ameuawa na
wengine watatu kujeruhiwa baada ya kutokea mapigano makali yaliyotokea Mashariki
mwa nchini hapa kati ya wapiganaji na waasi.
Msemaji wa UN
mjini New York, Farhan Haq ambaye hakutaja uraia wa wanajeshi waliouawa au
kujeruhiwa alisema wanajeshi hao wa UN walitumia ndege za helkopta kuwasukuma
nyuma wapiganaji wa M23 karibu na mji wa Goma, ambao ndio mji mkubwa zaidi
katika eneo hilo la Mashariki.
Mapigano hayo
yamekuwa ni mlolongo wa yale yaliyotokea mwaka 2012, baada ya waasi wa M23 kuuteka
mji huo kwa muda kabla ya kuondoka kutokana na shinikizo kutoka kwa jamii ya
kimataifa.
UN imetuma
kikosi maalum cha kijeshi cha (MONUSCO) kinachoshirikiana na kile cha serikali katika eneo hilo lenya utajiri mkubwa wa
madini kukabiliana na waasi hao.
Jeshi hilo
la Monusco limelazimika kufanya mashambulio ya anga na ardhini ili kuzuia waasi
hao wa M23 kukaribia mji wa Goma na ripoti zinasema mapigano makali yanaendelea
katika maeneo ya milima ya Kibati, takriban kilomita 15 Kaskazini mwa Goma.
Wapiganaji
wa M23 wamesema kuwa wanajeshi wa Congo na wenzao wa UN walifanya mashambulizi
ya anga na ardhini katika maeneo wanayoyadhibiti, Kaskazini mwa Goma.
BBC
0 comments:
Post a Comment