Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Wednesday, August 28, 2013

50 wauawa kwa kushambuliwa Iraq

BAGHDAD, Iraq
MASHAMBULIZI kadhaa ya mabomu yametokea nchini hapa na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 50 na wengine kujeruhiwa.
Polisi nchini humo wanasema kuwa mashambulizi hayo yalilenga ngome za Waislamu wa madhehebu ya Kishia wakati walipokuwa katika harakati za kwenda kazini huku wengine wakijishughulisha na mambo mengine.
Kiwango cha machafuko kimeongezeka nchini Iraq katika siku za hivi karibuni kutokana na uhasama unaoendelea kukithiri kati ya Waislamu wa Kishia na wale wa Wasunni.
Polisi wanasema kuwa zaidi ya milipuko 10 ya mabomu ilitokea wiki iliyopita katika maeneo mbalimbali ikiwemo Wilaya ya Jisr Diyala mjini Baghdad na mji wa Sadr.
Hadi sasa hakuna kundi lililojitokeza kusema kujihusisha na mashambulizi hayo lakini polisi wanashuku kuwa yalitekelezwa na wapiganaji wa Kisunni.
Waislamu wa Kisunni wanasema kuwa wanatengwa na serikali ya Waziri Mkuu Nouri Maliki ambaye anaongoza serikali ya Kishia tuhma ambazo serikali inapinga na kusema kuwa wapiganaji hao wanatumiwa na makundi ya kigaidi.
Tangu kuanza kwa mwaka huu, zaidi ya watu 4,000 wameuawa na wengine 10,000 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo ya mabomu.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa Julai ilikuwa mbaya kwa raia wa Iraq baada ya watu 1,057 kupoteza maisha yao wengi wao wakiwa mjini Baghdad.
REUTERS
Mwisho.

Operesheni ya kijeshi yanukia Syria bila UN
DAMASCUS, Syria
UWEZEKANO wa Umoja wa Mataifa (UN), kuidhinisha mashambulizi dhidi ya Syria ni mdogo sana, lakini tayari Marekani na washirika wake wanafanya maandalizi ya mashambulizi kupitia dhana ya uwajibikaji wa kimaadili.
Wiki moja baada kutokea shambulio linalodaiwa kuwa la kemikali kufanywa nchini Syria, mataifa kadhaa yameanza kupeleka vikosi kujiandaa na mashambulizi dhidi ya serikali ya Rais Al Assad.
Mwanzoni mwa wiki Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague alielezea uhakika kwamba gesi ya sumu ilitumiwa na vikosi vitiifu kwa rais Assad.
Tukio hilo linaendelea wakati uchunguzi wa karibu juu ya shambulio hilo unaendelea kufanywa na wakaguzi wa Umoja wa Mataifa.
Vikosi hivyo vinasubiri kauli ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa ambao iwapo watabainisha kuwa gesi hii ya sumu ilitumiwa na upande wa serikali, hakuna kitakachozuia mashambulizi ya kijeshi.
Muungano wa hiari
Kulingana na muktadha wa sheria hata hivyo, mashambulizi hayo yatakuwa yanakiuka sheria za kimataifa, kwa kuwa uhalali wake unaweza kutokana na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambako China na Urusi zinaweza kuzuia mpango huo kwa kutumia kura zao za turufu.
Kwa nchi hizo mbili, uingiliaji kijeshi kutoka mataifa ya nje siyo njia ya kuleta suluhu.
Kama litafanyika shambulizi la kijeshi, haitakuwa mara ya kwanza kwa Marekani kuchukua hatua kama hiyo pasipo idhini ya Umoja wa Mataifa kwani hata wakati wa utawala wa Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush, kupitia kile alichokiita muungano wa hiari, aliyaongoza mataifa kadhaa kuivamia Iraq mwaka 2003, kwa madai ya kuikomboa kutoka mikononi mwa Saddam Hussein.
Kabla ya uvamizi huo, Marekani ilijaribu kupitisha hoja yake ndani ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, kuonyesha kuwa kulikuwepo silaha za maangamizi nchini Iraq, ambapo waziri wa ulinzi wa wakati huo Collin Powell aliwasilisha ushahidi wa madai hayo katika baraza.
Hata hivyo, kulikuwa na mashaka makubwa kwa upande wa Ufaransa, Urusi na Ujerumani kuhusiana na ushahidi huo, na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Joschker Fischer, alieleza bayana kuwa hakuridhika na ushahidi wa Marekani.
Na kwa hakika mashaka yake yalikuja kutimia, baada ya kubainika kwamba ushahidi uliyowasilishwa katika umoja wa mataifa ulikuwa wa kughushi na Collin Powell alikiri kufanya makosa na kujiondoa katika ulingo wa siasa.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anakutana na maofisa wa juu wa serikalini na jeshi kujadili mikakati. 

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text