NAIROBI,
Kenya
ALIYEKUWA
mgombea wa nafasi ya urais, Peter Kenneth amesema kwamba kukua kwa deni la
taifa ni mzigo kwa Wakenya iwapo halitatafutiwa ufumbuzi kwa makini.
Kenneth, alisema
kwamba ukuaji wa deni hilo umekuwa kwa kasi ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2008,
ambako lilikuwa likifikia shilingi bilioni 700.
Alisema “Baada
ya kupita miaka sita deni limekua na kufikia shilingi trilioni 2 na hali inavyoonesha deni hilo litafikia kiasi
cha shilingi trilioni 2.5 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka,”
Aliongeza kuwa
“inawezekana miaka sita ijayo litafikia mara tatu, na hivyo kufanya asilimia 40
ya mapato kuelekea katika kulipa deni hilo,”.
Wakati wa
kampeini za mwisho za uchaguzi mkuu wa nchini hapa, Kenneth alikuwa akitoa
tahadhari ya hapo baadaye kukua kwa deni hilo la taifa.
Alisema kuwa
kabla ya kumalizika kwa kauli yake hiyo sasa hali imeanza kujidhihirisha kwa
deni la nchi hiyo kukua kwa kasi isivyo kawaida.
DailyNation
0 comments:
Post a Comment