HALI ya
sintofahamu katika kaunti ya Marsabit kaskazini mwa nchini Kenya imeendelea
kuwepo baada ya watu 20 kuripotiwa kuuawa kutokana na mapigano ya kikabila
yaliyotokea jana mchana.
Mapigano
hayo yemetokea miongoni mwa kabila la Borana, Gabbra na Burji yanaelezwa
kuchangiwa na mzozo wa ardhi na pia kuchochewa kisiasa.
Hata hivyo
polisi wamepelekwa katika eneo hilo la Marsabit kuimarisha usalama na kwa sasa
pole pole hali inasemekana kuendelea kurejea katika hali ya kawaida japo hofu
kubwa bado imetanda miongoni mwa wakazi kutokana na kuzuka tena kwa mapigano.
Muda mfupi
uliopita Amina Abubakar amezungumza na Sheikh Adan Wachu ambaye yuko katika
kamati ya kutafuta amani katika eneo hilo, kwanza anaelezea hali halisi ilivyo
katika eneo hilo kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment