Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Thursday, August 29, 2013

Obama: sijaamua kuishambulia Syria

WASHINGTON, Marekani
RAIS wa nchini hapa, amesema kuwa serikali yake imeshajiridhisha kwa taarifa za serikali ya Syria kutumia silaha za kemikali kwa kuwavamia raia wasiokuwa na hatia karibu na mji wa Damascus wiki iliyopita.
Obama amesema kuwa matumizi ya silaha hizo zimeathiri maslahi ya taifa la Marekani na huenda yakawa na matokeo mabaya kuhusu mgogoro huo wa Syria.
Hata hivyo, rais Obama amesema kuwa hajaamua ikiwa jeshi lake litaivamia Syria kijeshi siku moja baada ya azimio la Uingereza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutaka raia wa Syria kulindwa kushindwa.
Urusi ambayo ni mshirika wa karibu wa Syria ilipinga azimio hilo na kusema kuwa itaunga mkono azimio litakalosaidia kumaliza mzozo wa Syria Kidiplomasia na si vita.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon siku ya Jumatano alitoa wito kwa wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao ni nchi za Marekani, Ufaransa, Uingereza, Urusi na China walioungana na kuzungumza kwa sauti moja ya kutafuta njia ya kuiokoa Syria na kumaliza umwagaji damu.
Mpatanishi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo huo wa Syria Lakhdar Brahimi, naye amesema itakuwa sahihi kwa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Syria baada ya kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Wachambuzi wa siasa na usalama wanaona kuwa haitakuwa rahisi kwa azimio lolote linalolenga kuishambulia Syria kupitishwa kutokana na Urusi na China ambazo ni washirika wa karibu wa serikali ya Damascus.
Rais Bashar Al Assad amesema kuwa tishio la Marekani kuwa ikiwa uchunguzi utabaini kuwa silaha hizo zilitumiwa, italazimika kuingilia mzozo huo kijeshi ni jambo ambalo halikubaliki kamwe.
Mwaka uliopita, rais Obama alionya kuwa ikiwa serikali ya Syria itatumia silaha za kemikali dhidi ya wapinzani, nchi yake itaivamia kijeshi.
Machafuko nchini Syria yamesabisha zaidi ya watu 100,000 kupoteza maisha kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kwa mujibu wa takwimu za UN na mamilioni kusalia kuwa wakimbizi wakiwemo watoto.

REUTERS

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text