Drake kupiga kazi na baba yake
MSANII Drake anatarajiwa kumshirikisha baba yake mzazi katikia kazi yake inayokwenda kwa jina la 'Heat of the moment.' ngoma hiyo inatarajiwa kuwa katika albamu yake ya 'Nothing Wa The Same' anayotarajia kuiachia Septemba 24.
“Naishi katika ndoto za baba yangu kwani alinihitaji niwe mwimbaji maarufu, hiyo ni sababu iliyonifanya nimpende na anajua kuwa nampenda na kuwa ni rafiki yangu mkubwa." amesema Drake.
Bado haijawekwa wazi kama baba mzazi wa Drake, Dennis Graham ataimba kwenye ngoma hiyo au sauti yake tu ndio itakayoskika kama sample, kama kwenye ngoma ya zamani ya Drake “Jodeci Freestyle”aliyomshirikisha J. Cole.
0 comments:
Post a Comment