Dabo:
Nahitaji kutwaa tuzo nyingine
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya na mshindi wa Tuzo za muziki za Kilimanjaro nchini (KTMA),
kwa upande wa ragga mwaka 2012-03, Predator Dabo amesema kwamba anatarajia
kupata tuzo nyingine katika mashindano yajayo na kuendeleza rekodi yake.
Akizungumzia
kuhusu namna atakavyohakikisha analinda heshima yake hiyo ya kupata tuzo
nyingine msanii huyo amesema aliamua kukaa kimya pasipo kutoka kazi nyingine
ili asome mchezo na kuachia ngoma kali ambapo kwa sasa ameachia kazi yake mpya inayokwenda
kwa jina la ‘Niwe na wewe’.
Sababu
za kuipatia nafasi ya juu ngoma hiyo na kuitabilia kufanya makubwa inachangiwa na
kuitengeneza katika studio nzuri za One Love Fx chini ya mtayarishaji Tiddy
Hotter.
Msanii
huyo mwaka jana alipata tuzo hiyo akiwa ameingia kwenye kinyang’anyiro na wimbo
unaojulikana kama ‘Ganja man’.
0 comments:
Post a Comment