Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Monday, September 9, 2013

18 wauawa makabiliano na Boko Haram

TAKRIBANI watu 18 wamefariki kwenye makabiliano makali kati ya kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram na kundi la kijamii la kutoa ulinzi kwa raia, katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Vikosi vya Boko Haram 
Wengi wa wale waliouawa waliaminika kuwa vijana wanaotoa ulinzi kwa wanavijiji waliokuwa wanatoa ulinzi kwa mji wa Benisheik dhidi ya wapiganaji wa kiislamu.
Makabiliano hayo yametokea siku chache baada ya jeshi kufanya mashambulizi dhidi kambi za Boko Haram na kuwaua wanamgambo 50.
Boko Haram linataka kuwepo kwa sheria za kiisilamu kote nchini Nigeria.
Kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi mabaya tangu mwaka 2009, ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu.
Lakini mashambulizi ya aina hiyo yameongezeka zaidi katika siku za hivi karibuni licha ya jeshi kupeleka wanajeshi wake katika maeneo yaliyoathirika zaidi.
Katika kujibu ongezeko la mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo Mei, Rais Goodluck Jonathan alitangaza kuwepo kwa hali ya hatari katika majimbo matatu Kaskazini mwa nchi hiyo likiwemo jimbo la Borno.

Jeshi limeunga mkono ongezeko la makundi ya kutoa ulinzi katika majimbo hayo ili kukabiliana na Boko Haram.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text