Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Monday, September 9, 2013

Assad akana alitumia silaha za kemikali

RAIS Bashar al Assad wa Syria amekanusha kuhusika na shambulio la silaha za kemikali mjini Damascus mwezi uliopita.
Hayo aliyasema wakati alipokuwa akihojiwa na televisheni ya Marekani, CBS ambako alieleza, ikiwa serikali ya Rais Obama ina ushahidi kuwa alihusika, basi iutoe.
Rais Assad aliongeza na kusema kwa kujihamini kuwa iwapo Marekani itafanya shambulizi lolote washirika wa Syria watakuwa tayari kujibu shambulio lolote litalofanywa dhidi yao.
Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema Rais Assad amechagua wakati muafaka kwa mahojiano hayo, kwa sababu punde baraza la congress litaanza kujadili azimio kuidhinisha Marekani kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Syria.

Awali mwishoni mwa wiki mjini Paris Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, alisema mawaziri wenzake wa Jumuiya ya Kiarabu walikubali kuwa ikiwa Syria ilitumia silaha za kemikali, basi ilivuka mipaka ya viwango vya kimataifa.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text