Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, September 1, 2013

Ajali yaua watatu mkata

WATU watatu wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Mkata ikizihusisha gari mbili ambazo ni Toyota Hiace na Roli.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo kondakta wa Hiace hiyo alisema kuwa ajali hiyo ilitokea kutokana na uzembe wa dereva wake aliyekuwa anaendesha akiwa amelewa.
Kondakta huyo anasema kuwa wakati walipofika katika makutano ya barabara ya kwenda Segera na Makata ndipo dereva wake alishindwa kuiongoza gari yao na kujikuta akigongana uso kwa uso na Scania hiyo ambayo ilikuwa ikmitokea Arusha na kwenda Dar es Salaam.

Majeruhi hao akiwamo dereva wa Hiace aliyevunjika mikono yote wapo katika kituo cha afya cha Mkata kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text