Social Icons

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sunday, September 1, 2013

Obama aomba idhini ya bunge kuipiga Syria

WASHINGTON, Marekani
Rais Barack Obama kushoto na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon
ZIKIWA zimekatika zaidi ya wiki, Ikulu ya Marekani imekuwa ikielekeza mashambulizi yake kuelekea kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya nchi ya Syria, lakini hayo yamebadilika baada ya rais wa nchini hapa Barack Obama kutaka sasa baraka za bunge kuidhinisha hilo.
Uamuzi wa Rais Barack Obama wa ghafla wa kuomba ruhusa ya bunge unamuweka katika hatari ambayo inaweza kuharibu hali yake ya kuaminika iwapo hakuna hatua itakayochukuliwa kujibu shambulio la silaha za kemikali ambalo limekiuka kile binafsi alichokiita kuwa ni kuvuka ‘mstari mwekundu’.
Obama kuomba ruhusa ya baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican na baraza la seneti linalodhibitiwa na chama chake cha Democratic kukubali kuchukua hatua za kijeshi, suala ambalo tayari linaonesha utata ndani na kati ya vyama hivyo, inaifanya hali hiyo kuwa tete kuhusiana na jibu la Marekani katika mzozo wa Syria.
Mabadiliko hayo ya ghafla yanazusha maswali juu ya uwezo wa maamuzi wa rais na inaweza kuwafanya viongozi wa nchi hasimu za Marekani kama Syria, Iran, Korea ya kaskazini na kwingineko, kuvimba kichwa na kusababisha kujua kwamba rais wan chi hiyo hana nguvu ya kufanya jambo pasipo kupewa ruhusa.
Bunge la Marekani hata hivyo halitarajiwi kufanya vikao mapema mpaka Septemba 9, hali inayoonesha kwamba suala la Syria litakuwa la muda mrefu huku mauaji yakiendelea katika nchi hiyo.
Hakuna mtu ambaye analijua baraza hilo la Congress vizuri ambaye alikuwa tayari kutabiri kwa uhakika kile kinachoweza kutokea katika azimio la kuiruhusu nchi hiyo kuishambulia Syria lakini hali ya kutiliwa shaka inachangiwa kwa kiasi kikubwa na uhusiano mbaya uliopo kati ya Obama na bunge la nchini mwake.
Ufaransa yapata kigugumizi
Kama ilivyo kwa Marekani hata rais wa Ufaransa, Francois Hollande pamoja na kusema kuwa atamuunga mkono Marekani kuiadabisha Syria kijeshi naye hana ubavu wa kuiunga mkono nchi hiyo na kwenda vitani pasipo kupewa idhini na bunge lake.
Rais wa Urusi
Naye Rais Vladimir Putin wa Urusi anaziona tuhuma zinazotolewa na Marekani na washirika wake kuhusu serikali ya Syria kutumia silaha za kemikali ni za kipuuzi na hazina mashiko.
Anasema kuwa ni ngumu kulishutumu jeshi la Syria kutumia silaha hizo za sumu wakati tayari lilikuwa linasonga mbele na kutwaa maeneo yote yaliyokuwa yametwaliwa na waasi.
Putin alisema ikiwa Marekani ina ushahidi kuthibitisha tuhuma zake, basi ikabidhi ushahidi huo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Alimkumbusha Rais Obama kuwa aliwahi kutunzwa tuzo ya amani ya Nobel, na alimsihi kuwakumbuka wanyonge katika mashambulio na alikaribisha uamuzi wa bunge la Uingereza ambalo halikuunga mkono Uingereza kuingilia kati Syria, na anasema alishangazwa na uamuzi huo wa busara wa bunge.

0 comments:

 

Sample text

Sample Text

PATA HABARI NA BURUDANI MBALI MBALI POPOTE ULIPO!

Sample Text