Putin awaasa
wamarekani kuhusu Syria
RAIS wa
Urusi, Vladimir Putin ametoa ombi la moja kwa moja kwa raia wa Marekani kuhusu
mgogoro unaoendelea nchini Syria.
Putin
ameonya kwamba shambulio lolote la jeshi la Marekani dhidi ya Syria
litasababisha kuzuka kwa wimbi jipya la ugaidi na huenda likasababisha
kubadilika kwa mfumo mzima wa sheria na utulivu wa kimataifa.
Amesema kuwa
mamilioni ya watu wanaiona Marekani kama mfano wa taifa lenye demokrasia lakini
hutumia nguvu nyingi.
Hayo ameyasema
wakati ambao maofisa wakuu wa Marekani na Urusi wanatarajiwa kujadili yaliyomo
katika pendekezo la Urusi la kudhibiti kimataifa silaha za kemikali za Syria.
Wakati huo
huo kumekuwa na mapigano mazito nchini Syria katika kujaribu kuudhibiti mji
mkongwe wa kikristo Maaloula, licha ya taarifa zinazoeleza kwamba kikosi cha
serikali kiliudhibiti kutoka kwa wanamgambo wenye misimamo mikali ya dini ya
kiislamu.
Urusi ambayo
ni mshirika mkubwa wa rais wa Syria Bashar al-Assad, imependekeza kudhibiti
silaha za kemikali zilizo nchini Syria.
Japan
iliwahi kutumia silaha za kemikali dhidi ya wachina mwaka 1930, Mussolini
akatumia silaha hizo nchini Ethiopia wakati wa vita vya pili vya dunia huku
jeshi la Misri likitumia silaha hizo nchini Yemen miaka ya sitini.
Lakini yote
haya hayawezi kufananishwa na kilichotokea eneo la Halabja. Machi mwaka 1988,
aliyekuwa rais wa Iraq Saddam Hussein aliamuru kutumiwa kwa gesi ya sumu dhidi
ya wakurdi na kuwaua watu zaidi ya 5,000 papo hapo.
0 comments:
Post a Comment