AU kujiondoa ICC
ADDIS
ABABA, Ethiopia
VIONGOZI
wa Afrika (AU), wanatarajiwa kukutana mwezi ujao mjini hapa, kujadili msimamo
wa bara hilo kuhusu iwapo watajiunga na Kenya katika hoja ya kujiondoa kwenye Mahakama
ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Mkutano
huo unatarajiwa kufanyika kutokana na ombi la Kenya kutaka kikao cha dharura
cha AU kujadili kesi zinazowakabili Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William
Ruto.
Kuna
taarifa zinaeleza kuwa ombi hilo la Kenya lina dalili za kuungwa mkono na
mataifa mengi barani Afrika ambao wamekuwa wakiilalamikia mahakama hiyo
kuegemea zaidi kwa viongozi wa bara hilo.
Tangu
kuanza kwa kesi ya Makamu wa rais wa Kenya William Ruto, ICC wiki iliyopita, na
ile ya Rais Kenyatta inayotarajiwa kuanza Novemba, dalili zimeonekana kuwa
wengi hawana imani na mahakama hiyo wakiiona kama chombo cha nchi za Magharibi
kukandamiza waafrika.
Kikao
cha dharura kimeitishwa kujadili suala hilo baada ya Kenya kuonekana kutaka
kuungwa mkono katika azma yake ya kujiondoa ICC.
Kuna
uwezekano wa nchi wanachama wa mkataba wa Roma kujiondoa ICC lakini bado kuna
nafasi ya maombi mengine kufanywa kuhusiana na hilo.
0 comments:
Post a Comment